Msaada: Ninataka kuanzisha kikundi cha wanaume

Msaada: Ninataka kuanzisha kikundi cha wanaume

mahadhialy

Member
Joined
Oct 19, 2019
Posts
45
Reaction score
24
Habari zenu ndugu zangu

Mimi nimepata idea ya kuanzisha kikundi cha wanaume. Kikundi hicho kitamhusu mwanaume pamoja na jamii. Kikundi hiki kitaanzisha miradi mbalimbali kwa mfano viwanda, mashamba n.k. ilimradi tupunguze ukosefu wa ajira katika jamii lakini mambo yakienda sawa kikundi kitamiliki hospitali, shule n.k.

Pia itapunguza mababa kutelekeza familia zao kwasababu ya ukosefu wa ajira pamoja na umaskini. Kwahiyo ninaomba msaada jinsi gani nitakisajili kikundi kisheria.

Mnatakiwa muwe watu wangapi ili mpate kukisajili hicho kikundi? Na pia kwa yeyote anaetaka tushirikiane karibu sana mimi nipo Dar
 
Nikutie moyo ndugu, wote wanaokukatisha tamaa hawajui chochote Cha kukusaidia
Kwanza kikundi ni Bora kikawa na jinsia zote, na has a ikijumuisha utofauti was umri yani awepo mmama, wadada na wanaume, japo mmama ni optional kinaweza kuwa kikundi Cha vijana tu,

Ukishapata vijana kumi andaeni katiba yenu nendeni kwa wataalam Kama hamna uwezo huo nyie wenyewe Kisha muwasilishe maombi ya kusajiliwa kwa mtendaji was kata, mkiambatanisha vitambulisho vyenu pamoja na utambulisho was mwenyekiti was Kijiji kuwa anawafahamu. Mtalipia elfu hamsini halafu baada ya wiki 2 mtapata cheti,

Kwa cheti hicho kwa kuanzia mnaweza kwenda sido kupata mafunzo ya usindikaji viwandani Kama hamna wazo, ama mkiwa na wazo lenu ni vyema moajichanga kiasi chochote mkaanzisha kitu chochote ambacho hata Kama kitawaingizia elfu kumi itakua vyema.

Fursa zilizopo mnaweza kwenda halmashauri kuomba mkopo kwa kuanzia mtapewa m5 mkiilipa vyema mtaongezewa, Kuna vijana nawafahamu just juzi wamepewa mkopo was m30 baada ya kuwa walipaji wazuri

Fursa nyingine mnaweza kuomba tenda kadhaa wa kadha zinazotangazwa nanhalmashauri ikiwemo ukusanyaji was taka, ukusanyaji was ushuru was masoko, parking nk.

Chamsingi nikushauri uwe na Nia, tafuta wenye Nia, na msikate tamaa ingiza mguu na usiache,
Goodluck
 
Ni pm tuzungumze
Habari zenu ndugu zangu

Mimi nimepata idea ya kuanzisha kikundi cha wanaume. Kikundi hicho kitamhusu mwanaume pamoja na jamii. Kikundi hiki kitaanzisha miradi mbalimbali kwa mfano viwanda, mashamba n.k. ilimradi tupunguze ukosefu wa ajira katika jamii lakini mambo yakienda sawa kikundi kitamiliki hospitali, shule n.k.

Pia itapunguza mababa kutelekeza familia zao kwasababu ya ukosefu wa ajira pamoja na umaskini. Kwahiyo ninaomba msaada jinsi gani nitakisajili kikundi kisheria.

Mnatakiwa muwe watu wangapi ili mpate kukisajili hicho kikundi? Na pia kwa yeyote anaetaka tushirikiane karibu sana mimi nipo Dar
 
Hivi aliebuni mchoro na mfumo wa gari kwa ujumla (kipindi hamna magari kabisa duniani) angekatishwa tamaa na kushambuliwa kama hivi kweli leo tungekuwa na magari

Waafrika hatujui kila kitu lakini ni wajuaji,vere eksaitingi[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Back
Top Bottom