MSAADA: Nini dawa ya chunusi usoni?

Acha mihemko we pimbi, chunusi ni tatizo sensitive kuliko unavyodhani...as for your case labda ilikua uchafu but sio kwa watu wote iko hivyo.
 
Tumia facial wash zipo za aina nyingi ila kuna inaitwa Acne facial wash ni nzuri sana

Kwa ushauri wa ngozi karibu PM
 
Chunusi za sumbua je, Tiba yake ni nini?
Usafi wa mashuka na mito ndio kitu cha kwanza kabisa,kuosha uso mara mbili hadi tatu kwa siku kwa kutumia sabuni maalum ya kuondoa mafuta usoni muhimu sana,. Usafi wa simu Yako pindi unapoiweka usoni kuzungumza
Kingine ni hivi kunywa maji mengi , nifanyie scrub kwa mwezi mara moja ...... Tafuta serum inaitwa Disaar ya vitamin c
 
Nahtaji msaada Nina chunusi zisizoisha ,rashes dark spots Kila nacho tumia siku za mwanzo kinanikubali lkn ikipita wiki tu natokwa tena n chunusi
Duh nmechoka kwakweli
 
Wakati nabalehe chunusi zilinitokea ila baada ya muda mfupi ziliisha zote haikubaki hata kipele kimoja hadi leo, sijui dawa niliyotumia ila nakumbuka
ziliisha wakati nilijichanganya sehem moja nikawa nafanya mazoezi makali sana kwenye jua na kuvuja jasho jingi kila siku na kunywa maji mengi, usiku nilikua nikioga sijipaki mafuta alfajiri naamkia mazoezi
Zilivyopotea hazikuwahi kurudi Hadi leo na hata hayo mazoezi sifanyagi tena
 
Nahtaji msaada Nina chunusi zisizoisha ,rashes dark spots Kila nacho tumia siku za mwanzo kinanikubali lkn ikipita wiki tu natokwa tena n chunusi
Duh nmechoka kwakweli
Pakaa Colgate dawa ya Meno ina kausha na ngozi inarudi kua kawaida, pakaa kaa nusu saa suuza uso wako vitakauka na kupotea

Acha kupaka mafuta mengi usoni, unapotokwa na majasho kwenye mizunguko, tumia Dettol kusafisha uso wako
 
Chunusi za sumbua, je, tiba yake ni nini?
Inapokuja juu ya suali la chunusi hakuna dawa inayoweza kumtibu kila mtu, dawa itakayomfaa mtu mmoja haitomfaa mtu mwengine, Ushauri wangu ni kwanza kamuone daktari bingwa wa ngozi- dermatologist akupe ushauri na hata anaweza kukufanyia test mbali mbali na kukushauri dawa za kujaribu. Pia jaribu kutumia sabuni ya dove watu wengi wanasema inasaidia kukausha chunusi na kupunguza nguvu zake. Uwe unakosaha uso kwa kutumia maji ya room temperature angalau kwa mara tatu kwa siku. Usitumie makeup kali na chagua moja na sio kila siku kubadili badili. Hakikisha unakuwa na face towel unazotumia wewe tu na uhakikishe uanzifua mara kwa mara. Pia uwe unabadili na unakosha cover za pillows zako kila mara. Ukiamua kutumia dawa yeyote ile basi dumu nayo kwa kipindi uone mabadiliko yake na sio kubadili dawa kila siku mtu anaposema dawa fulani ni nzuri zaidi.

Kama huna dawa unayotumia regurlarly kwa sasa hebu jaribu gel inayoitwa acneside uone kama itakusaidia, i hope inapatikana huko tz
 
Alokwambia wazungu hawana chunusi ni nani? Na kwa nini kila kitu mnalinganisha na wazungu? Nenda google na search facial acne uone picha za hao wazungu wako walivyo na acne tele wanaume na wanawake.
Shukran kwa kunisaidia kujibu, maana ushamba ni mzigo!
 
Usipaka mafuta yenye oil, usipaka mafuta ya mgando usile karanga mbichi kwa wengine zinaharibu ngozi huleta vichunusi
Paka lotion changanya na mate kidogo ndiyo upake, kabla ya kulala paka mate usoni ndiyo ulale matokeo ni kabla ya wiki
 
AAAA sasa huo ni uchafu wa mwisho! kupaka mate usoni alokwambia ni dawa ya chunusi ni nani? Hizi idea za gengeni jamani tuacheni maana nimeona watu wanashauri kupaka damu ya period, shahawa na sasa mate! come on this is too much!
 
Ni uchafu kivipi mkuu?
Na unachobisha hapo ni nini
Nimekwambia before wiki kuisha hautakuwa na hivyo vichunusi unakataa kwamba umefanya na hujapata matokeo au kuna mtu ameombwa hela kwamba unaogopa kutapeliwa?
 
Hivi kiswahili ni lugha yako? Mambo ya kutapeliwa yamekujaje hapa? Hivi wewe ni mtu wa asili gani ya kuwa huoni kuwa kujipaka mate usoni si uchafu? Una proof gani kuwa mate ni dawa ya chunusi? Usikae huko uliko na kudanganya watu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…