Msaada; Nini maana halisi ya Jasusi?

kzba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,355
Reaction score
789
Kitambo kabla cjawa baba nilikuwa najua mtu ukimwita jasusi ni jambazi lililoshindikana, baadae tena naanza kujifunza kingereza neno jesus nilikuwa natamka jasusi hapo ndo nilizidi kupagawa lakini niwe muwazi tu hadi hivi leo sijajua maana halisi ya neno jasusi au hao majasusi ni akina nani
Msaada waungwana

Nawasilisha.
 
Nijuavyo Mimi Jasusi Ni Mpelelezi Kwa Maana Ya 'Spy'
 
Jasusi ni mpelelezi wa hali ya juu anayeweza kuingia mahali popote bila kuonekana. Ni kweli neno hilo limetokana na jina JESUS kwani naye Alikuwa na uwezo huo, ikiwemo kuingia duniani kimiujiza
 
Jasusi ni mpelelezi wa hali ya juu anayeweza kuingia mahali popote bila kuonekana. Ni kweli neno hilo limetokana na jina JESUS kwani naye Alikuwa na uwezo huo, ikiwemo kuingia duniani kimiujiza

Siyo kweli anaingia popote bila kuonekana Bali anaingia popote bila kujulikana Kama mpelelezi Lakin watu wanamuona siyo kwamba haonekani
 
Mkuu Nikupe fundisho dogo tu... Neno Jasusi ni neon limetokana na neon la kiarabu "jasus" Sasa maana ni Mtu mweye kuwa na uso mbili (wasemavyo wenyewe) Yaani mtu huyo hukuonesha uso wa kupenda na uso wa kukutangaza !! Yaani Mnafiki anaiishi na wewe lakini siri zako anapeleka kwa muingine huko. Mfano nchi hutuma vijana wake kuenda kusoma nje,, Sasa wakati huo huo kati yao hao vijana huamrishwa mmoja kuleta repoti za wenzao nchini kwa walokuwa nje !! Hivyo huyu kijana ana jasisi mwenendo wa wenzao !!
 

Hapa utadanganywa sana chamsingi kama kalugha ka watu kanapanga tafuta vitabu vya introduction to Espionage and intelligence basii utaelewa maana halisi ya Jasusi mkuu
 
Hapa utadanganywa sana chamsingi kama kalugha ka watu kanapanga tafuta vitabu vya introduction to epstionage and intelligence basii utaelewa maana halisi ya Jasusi mkuu

Hapo sasa ndo mtihani mdau
Kusoma naweza ila kuelewa ndo empty kabisa kudadadeki
 
Hapa utadanganywa sana chamsingi kama kalugha ka watu kanapanga tafuta vitabu vya introduction to epstionage and intelligence basii utaelewa maana halisi ya Jasusi mkuu


Bila Shaka Wewe Umeshasoma Hivyo Vitabu, Unge eleza Japo Kwa Ufupi Ulichojifunza(ukweli) Badala Ya Kumuacha Adanganywe Hapa.
 
hahaaaaahaaa jf raha sana haya mkuu pole sana

Sawa kaka nitajitahidi hivyo hivyo kuvitafuta na kusoma kwa msaada wa shemeji yako manake yeye alhamdu lilah kidogo na ka degree kake ka makerere ataokoa boti Nungwi kaka
 
Bila Shaka Wewe Umeshasoma Hivyo Vitabu, Unge eleza Japo Kwa Ufupi Ulichojifunza(ukweli) Badala Ya Kumuacha Adanganywe Hapa.

Ndio tatizo letu watanzania tunapenda kila kitu tutafuniwe mkuu any way sijui tafuta vitabu na dictionary mbona zipo kibao zinaelezea Espionage nini mkuu
 
kwa uelewa wangu wa elimu ya mtaani jasusi ni mpelelezi wa kimataifa aliyepata mafunzo ya upelelezi, au ata ukomandoo mwenye kuweza kutumia mbinu nyingi za kufuatia jambo fulani, some time wanaweza ata kujifanya kichaa akiwa anafuatilia jambo
kishwahili fasaha huitwa shushushu
 
kwa uelewa wangu Jasusi ni mpelelezi wa level ya kimataifa kwa maana anapeleleza habari za siri(nyeti) za taifa moja kwa faida ya taifa ya lingine.

Huyu ana tofauti na kachero ambaye ni mpelelezi wa ndani mfano wapelelezi wa jeshi la polisi.
 
Hapo sasa ndo mtihani mdau
Kusoma naweza ila kuelewa ndo empty kabisa (kudadadeki)
Kwa namna ulivyomalizia tu na hilo neno (kudadadeki)psychologically inaonesha kuwa unafahamu kitu ila tu upo hapa kutaka kutuzuga mkuu.
 
I dont know who you are and i dont know what you want.If you are looking for ransom I CAN TELL YOU i have no money what i do have are particular set of skills i have acquired over a long career skills THAT MAKE ME A NIGHTMARE for people LIKE YOU.If you let my daughter go.....
Ukishindwa kusoma vitabu husika jaribu filamu basi mf:TAKEN,007,SAFE HOUSE nk
 
jasusi n mtu mpelelezi ambaye hana mfumo kaz maalum huwa ana baadilisha mazingira hana utambulisho wa kuaminika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…