Ni vigumu mwanamke kuangukia katika tarehe moja kwa kuwa mzunguko wa hedhi haufuati kalenda ya mwezi bali mzunguko wa mwanamke, na miezi hutofautiana urefu so sio rahisi kufuata tarehe hiyo hiyo japo yaweza tokea concidentally kwa mtu ambaye hana constant cycle kama mkeo.
Naona watu wengi wanazungumzia siku ya 14 toka mtu ameanza mzunguko ndio huwa siku ya hatari. Hii ni sawa kwa mwanamke mwenze mzunguko wa siku 28 zisizobadilika. Mzunguko wa hedhi una sehemu mbili kubwa, sehemu ya kwanza huanza kuanzia kuanza hedhi mpaka yai kupevuka (follicular phase), na sehemu pili ni baada ya yai kupevuka mpaka kupata tena hedhi(luteal phase). Sehemu ya kwanza hubadilika badilika kutegemeana na urefu wa mzunguko wa mwanamke husika na sehemu ya pili ndio huwa constant yaani huchukua siku 14, kwa hiyo siku za kupata ujauzito (fertility days, wengi huita danger days sijui kwa nini ni danger) ni siku 14 kabla ya kuanza hedhi na si siku 14 baada ya kuanza hedhi. Ukitaka kufanya hesabu za kujua lini mkeo au mwenza wako anaweza kushika ujauzito, tafuta urefu wa mzungo wake halafu toa 14, siku utakazopata ndio utahesabu kuanzia anapoanza hedhi na ndio itakuwa siku ambayo yuko fertile. Mizunguko ya hedhi ya kawaida inaanzia siku 21 mpaka 35, kwa hiyo kama mtu ana mzunguko wa siku 21 ukitoa 14 zinabaki siku 7, kwa hiyo huyu atakuwa fertile siku ya 7 toka ameanza hedhi na si siku ya 14 kama ilivyozoeleka. Mtu mwenye mzunguko wa siku 35 ukitoa 14 atakuwa fertile siku ya 21. Mtu mwenye mzunguko wa siku 28 ukitoa 14 inabaki 14, atakuwa fertile siku ya 14 toka ameanza hedhi. kwa hiyo ni wale wenye mzunguko wa siku 28 ndio huwa fertile siku ya 14 toka kuanza hedhi. Natumaini nimesomeka.
Kwa issue ya mkeo, japo sijui umri wake lakini mzunguko usio sawa (irregular cycle) una changamoto sana katika kukadiria siku ambayo yuko fertile. Kwa mizunguko yake ilivyo anaweza kuwa na tatizo hivyo unaweza kuwaona wataalamu (gynaecologists) wakakusaidia kufanya uchunguzi wa kwa nini cycle yake iko irregular, na wakakusaidia kuirekebisha na hivyo mkaweza kufanya makadirio sahihi ya siku yake ambayo yuko fertile. Japo mtu mwenye cycle isiyo regular pia anaweza kuwa na matatizo ya upevushaji mayai (ovulation).
Hata hivyo unaweza kutumia njia nyingine kujua mkeo kama amekaribia kuengua yai (ovulation) kama kutumia ovulation test strips, kuangalia mabadiliko ya ute ute ukeni na kuangalia mabadiliko ya joto la mwili. Pia ni muhimu kutrack siku zake kama unavyofanya, zitamsaidia daktari wako namna ya kukusaidia.