Msaada: Nitapata wapi hospital ya mifupa tofauti na MOI?

Msaada: Nitapata wapi hospital ya mifupa tofauti na MOI?

nenda kibaha,tafuta dr kiwelu.usiende kwa bake atakuwekea chuma ambazo hazifai baadaye utajikuta unaingia kwenye hasara
 
.....popote pale uendako Dr. Mboya kwenye ishu zinazohusu Mifupa ni mwisho wa matatizo: jamaa ni mtaalamu(ni Daktari Bingwa) haswaaa. Anapatikana MOI na pia unaweza kumpata Kairuki Hosp-Mikocheni(pale huwa ana clinic siku ya J'mosi) kama vipi ni PM nikurushie namba yake ya simu.

Mkuu naomba namba ya Dr Mboya
 
Nenda KCMC kwenye Idara ya Upasuaji mifupa.. inasifika sana kwa huduma zake pia unaweza kumpata Daktari Bingwa wa mifupa anaitwa DR MANDARI
 
Kuna jamaa anatibu kwa dawa za miti shamba na anatibu vizuri sana mpaka una shangaa, nina ndugu yangu alivunjika nyonga aliangukiwa na kifusi machimboni huko Tanga, baada ya kuzungushwa sana muhimbili akaelekezwa na ndugu wa mgonjwa mwingine aliewahi kutibiwa huko, jamani ni ajabu lakini kweli, mgonjwa alikuwa anabebwa tu maana nyonga ilichomoka mguu ukawa una zunguka lakini baada ya kuanza hayo matibabu ndani ya mwezi mmoja akaanza kutembea mwenyewe, na sasa anaenda na ki babaji tu kujichukulia dawa tena peke yake.
 
Back
Top Bottom