Kuna jamaa anatibu kwa dawa za miti shamba na anatibu vizuri sana mpaka una shangaa, nina ndugu yangu alivunjika nyonga aliangukiwa na kifusi machimboni huko Tanga, baada ya kuzungushwa sana muhimbili akaelekezwa na ndugu wa mgonjwa mwingine aliewahi kutibiwa huko, jamani ni ajabu lakini kweli, mgonjwa alikuwa anabebwa tu maana nyonga ilichomoka mguu ukawa una zunguka lakini baada ya kuanza hayo matibabu ndani ya mwezi mmoja akaanza kutembea mwenyewe, na sasa anaenda na ki babaji tu kujichukulia dawa tena peke yake.