Msaada: Nyumba ya contemporary inavuja

Hizi hata kama fundi ni mtaalamu sana,inataka kila baada ya miaka kadhaa fundi akakague huko juu na kuziba baadhi ya maeneo,kifupi kwa miji inayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka lazima ulie...
 
Tafuta fundi mzuri kwa kupaua. Ukiweza kuwatembelea nabaki africa wana mafundi wamewatrain. Pia nabaki wana gundi zote na material yote kwa ajili ya Waterproofing eg synroof kwa ajili ya bati na kuta zinapokutana. Fundi wa kujenga na kupaua ikiwezekana wawe tofauti. Maana si kila fundi wa kujenga anajua kupaua.
 
Ukute aliyejenga hapo ni engineer tena mwenye master😜! Utajiteteaje bwashe😂!
 
Mie siyo fundi, ila kosa lipo kwenye drainage! Drainage ziliwekwa juu ya floor ambayo pia haiko even na hivyo maji yanatuwama na kuweka bwawa, what do you expect😜 embe chini ya mnazi🤷? Hivyo imesafirishwa hiyo siyo ya mnazi😂!
 
Kama umejenga contemporary house, kwa kuepuka "gharama" lazima ulowane...siyo cheap kabisa kuficha paa, kwa nyumba kubwa jiandae kutoboka

Pia, Design ya kumwaga maji ndio inawaumiza wengi, unakuta maji yote yanatotoka kwenye bati yanakusanywa sehemu moja

Kwa design kama hii hapa chini kulowana ndani sahau ila lazima utoboke
 
Acha kudanganya watu haijanzia msumbiji na hata Hali ya hewa unayoizungumzia sio kweli .Msumbiji iko ukanda mmoja na mikoa ya mtwara Lindi na ruvuma na kwa upande wa Msumbiji ni mikoa ya cape Delgado Hadi Beira eneo hili Lina mvua nyingi sana hasa kuanzia Mwez Nov Hadi April ,so tatizo mvua tatizo mafundi wetu bado aina hii majengo ni ngeni kwao .
 
Nilikuwa nazipenda sana nyumba za aina hii hadi nilipojionea kwa ndugu yangu.

Nyumba imeezekwa lakini inavunja sana Pembeni mwa mabati.

Afanyeje ili isivuje?

N.B: Pembeni ukuta umechimbwa ili kuingiza bati na kuzibwa kwa cement ya water proof.
Pole kwa hiyo changamoto,

Unaweza kutembelea mtandao wa UWEKEZAJI MAJENGO..


Hapa utajifunza mambo ya msingi kuhusu uwekezaji kwenye majengo.
 
Mambo ya kufata Mkumbo! Dodoma wanalia sana walojenga contemporary!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Mimi nilitaka kujenga hivyo ila nikapata washauri wakaniambia niachane nazo, nyumba nyingi zinasumbua kuvuja au kulowesha ukuta
 
Exactly
 
Na hapa ndipo hoja kuu ilipo. Ujenzi wa nyumba hizi ukizingatia taratibu ni very expensive, Kwanza hata ile ya zege, inapaswa kuweka kwa ratio kali sana na vipimo maalum inayozuia hata tone moja la maji kupenya kwenye hiyo zege, sasa watu wanaweka zege ratio ya kawaida kisha wanapiga eti plasta ratio kali!! Hapo tu washafeli! Ujenzi wa lile gata la zege unaweza gharimu fedha sawa na gharama ya kuinua nyumba kutoka kwenye msingi hadi kwenye lenta kama likijengwa inavyotakiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…