Msaada: PC system inakula sana data

February Makamba

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2020
Posts
2,151
Reaction score
2,983
Beijing!
Bonjour wakuu, PC yangu inakula sana data kwa vitu visivyoeleweka.
Nimeweka connection kuwa metered
Nimestop background applications
Nimestop google updates (ilikuwa ishakula mb95)
Nimeweka data limit
Nimezuia system updates mpaka January huko

Lakini bado kila mkitumia nakuta Mb kibao zimeenda nikiangalia nini kimekula naambiwa ni system
Hii hapa screenshot baada ya kuanza kumonitor data usage kwa nusu saa
 
Mkuu mb 411 kwa siku 12 mbona kama kawaida tu.

Unaweza ukaweka firewall kitu chochote kisiingie internet bila ruhusa yako
Mkuu hizo Mb ni leo tu, tena ndani ya nusu saa...hiyo imeangalia ndani ya hizo siku lakini mimi sijawahi kuiunga na internet mwezi huu wote.
Hiyo firewall nawekea wapi? Kwenye settings au?
 
1. Nenda sehemu ya SEARCH andika SERVICES

2, Ikifunfuka tu chagua RUN AS ADMINSTRATOR

3. Ikifunguka tu, chuka chini kabisa utaona list imeandikwa WINDOW UPDATE

4. Bonyeza hapo kisha kuna kuna sehemu utaona pameandikwa MANUAL ingia hapo kwa kubonyeza OK

5. Chagua DISABLE, kisha bonyeza APPLY kisha OK



#RudiNyumbaniKumenoga
 
Mkuu mbona sioni io run as administrator
 
Mimi nina fikiri kuna Program zina jifunguwe wenyew wakati wewe unapo funguwa PC yako hebu bonyeza Ctrl +Alt pamoja na Del ipate kufunguka Task Manager ikisha funguka hiyo Task Manager nenda mahali palipo andikwa Startup zuia aka Disable baadhi ya program zinazo funguka wenyewe lakini usije ku disable anti-virus unaweza ku disable CCleaner, Java Updates Helper , Nero kama unayo Skype , Camera aka Vimico ,Adobe reader , google Updates, na program za Apple hiyo itakusaidia kupunguza MB zako zisipate kuliwa kwa wingi .
 
Mkuu hizo Mb ni leo tu, tena ndani ya nusu saa...hiyo imeangalia ndani ya hizo siku lakini mimi sijawahi kuiunga na internet mwezi huu wote.
Hiyo firewall nawekea wapi? Kwenye settings au?
Firewall mfano wake ni hio Glasswire aliokutajia mdau, window inakuja na firewall yake ila sio powerfull hivyo unadownload 3rd party firewall ili kupata options nyingi.
 
Asante sana mkuu.
 
Kituo hapa nichukue madini Nina surface pro 3 inakula data Hadi naogopa kutumia
 
Zima auto updates za Windows, Disable Microsoft Windows Defender, Zima background apps.... Utaona mabadiliko, PC yangu naweza tumia hata MB100 kwa siku 1 au 2 na peruzi tu JF na websites mbali mbali kwa Chrome na zikiisha zinaisha ki halali kabisa na apps ntakayokuta imezitumia ni Chrome pekee sio nje ya hapo....
 
Tumia program inaitwa CCleaner itakusaidia kuzuia program ambazo zinakula bando pamoja na zinafunguka na kutumika bila wewe kujua utaweza kuzuia [emoji2937]

Iko Poa Sanaa CCleaner
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…