Kizamani
Tulikuwa tunabofya hapo pa kuwashia na kushikilia kwa sekunde kama 6 hadi 10 hadi pc izimike. Kisha unawasha tena kuangalia kama tatizo lipo.
Kama bado lipo, tulikuwa tunaunganisha waya wa VGA kwenye monitor nyingine na kubofya kitufe cha kuhamisha display kuonesha kwenye monitor hiyo nyingine.
Kama bado haioneshi, tulikuwa tunapeleka kwa fundi.
Mafundi walikuwa wanatuambia huenda mainboard imekufa, ama display imekufa, kama ni board imekufa, usihangaike kuitengeneza, bali toa harddisk ili ufanye backup ya data zako kisha pc utaitumia kama spea.
Kama ni dispaly, ni rahisi kubadilisha nyingine zinazoingiliana.
Kila la heri.
Vijana wa sasa watakusaidia kisasa zaidi.