ALU anaweza tumia kama mimba ina wiki 15 na kuendelea (yaani second trimester na kuendelea), haina madhara kwa mtoto kwa mimba yenye ukubwa huo, mimba changa haishauriwi kutumia dawa hiyo kwa sababu haijathibishwa kama ni salama wakati ambapo viungo vya mtoto vinajiunda. Vinginevyo atumie quinine ambayo ni safe kuanzia mimba changa mpaka kubwa.
Hospitali bado wanatoa SP kwa wajawazito, kwa ajili ya kumkinga mama lakini kwa sasa haiwi recomended kuitumia kwa tiba. Malaria ni mbaya sana kwenye ujauzito, mtibu mkeo mapema.