Msaada please!

Msaada please!

Read me

Member
Joined
Jan 10, 2011
Posts
35
Reaction score
4
Habarini wana jf!
Naomba kujua je mama mjamzito kama amepata maleria anaweza kutumia hii dawa mseto ya maleria (ALU)?,
Je kuna madhara yoyote anaweza kuyapata mama au mtoto aliye tumboni?
Ni dawa ipi inafaa kwa mama mjamzito kwa kujitibu na maleria.
Natanguliza shukrani za dhati.
 
ALU haifai kwa mjamzito ebu wahi hospitali utapata tiba inayofaa ni hatari sana kubugia dawa bila kuonana na watalaamu.
 
ALU anaweza tumia kama mimba ina wiki 15 na kuendelea (yaani second trimester na kuendelea), haina madhara kwa mtoto kwa mimba yenye ukubwa huo, mimba changa haishauriwi kutumia dawa hiyo kwa sababu haijathibishwa kama ni salama wakati ambapo viungo vya mtoto vinajiunda. Vinginevyo atumie quinine ambayo ni safe kuanzia mimba changa mpaka kubwa.

Hospitali bado wanatoa SP kwa wajawazito, kwa ajili ya kumkinga mama lakini kwa sasa haiwi recomended kuitumia kwa tiba. Malaria ni mbaya sana kwenye ujauzito, mtibu mkeo mapema.
 
habarini wana jf!
Naomba kujua je mama mjamzito kama amepata maleria anaweza kutumia hii dawa mseto ya maleria (alu)?,
je kuna madhara yoyote anaweza kuyapata mama au mtoto aliye tumboni?
Ni dawa ipi inafaa kwa mama mjamzito kwa kujitibu na maleria.
Natanguliza shukrani za dhati.

tafuta ushauri wa madaktari nenda hospitali usimpe alu, inategemea na semester aliyopo, nenda hospitali
 
Nikushauri tu mkuu nenda hospitali waganga watakupa maelekezo mazuri!
 
Nenda hospital kwanza umejuaje kama unamalaria?? Umekwenda hospital?? Hawajakushauri dawa ya kutumia???

Pole kama hujakwenda hosipital fanya haraka tena hima uende
 
Habarini wana jf!
Naomba kujua je mama mjamzito kama amepata maleria anaweza kutumia hii dawa mseto ya maleria (ALU)?,
Je kuna madhara yoyote anaweza kuyapata mama au mtoto aliye tumboni?
Ni dawa ipi inafaa kwa mama mjamzito kwa kujitibu na maleria.
Natanguliza shukrani za dhati.

Sure zipo dawa ambazo si nzuri kabisa kwa mimba,kwa ALU mi sina uhakika. But Dont worry,Madaktari wote ambao professionally wako okay,they know......huwa lazima wamwulize mgonjwa wa malaria wa kike (alie ktk age ya kushika mimba) KAMA ANA MIMBA AU LA. Wanafanya ivo ili kama atakuwa na mimba na malaria,hii itawasaidia kutoa dawa sahihi!! Au just tell your doctor kuwa pamoja na kuwa una mimba vilevile una malaria ili waku-treat accordingly.
 
Nawashukuru nyote kwa mawazo yenu mazuri mliyonipa,
huo ushauri wenu mmetoa nitaufanyia kazi.
Mbarikiwe wote wana jf.
 
Hili jambo si la kujadili kila mtu. Nachokushauri wahi hospitali. Na uache tabia yako ya kuganga watu nyumbani.
 
Back
Top Bottom