mambo dada joy?
Sie wadada huwa tunapenda sana kuwa na mwenzi mmoja mzuri mwaminifu kwa maisha yote yaliobakia. Tunapenda huyo kaka atupende kwa ukweli, awe hendasome, awe na akili, ..... Na listi ndefu sana.
Ila inapofika siku ya kusema yes/no huwa tunapata vigugumizi, kwani mara zote unakuta hajatimiza hata nusu ya listi tulionayo kichwani na katika ndoto zetu. Au anakuja wakati mbovu.
Ni wakati mgumu.
Pole sana dada.
Cha muhimu jiamini kama mwanamke uliepewa 'instincts'
fuatilia maadili uliofundishwa tangu utotoni, hakuna cha kuhesabu miezi wala miaka.
Kama unamuamini sasa, unamuheshimu na mawazo yake kwa sasa, chances ni kuwa itakuwa hivyo kwa muda mrefu ujao.
Ila kama una sita, kwa kutazama yeye (sio muda) basi ni kweli kuna tatizo, ila mueleweshe uliza, akukujibu ukaridhika basi mama karibu kwenye chama.
Tegemea atabadilika sana, na wala sio kwamba alikuwa anajificha (mostly) bali anazidi kukua kama wewe utakavyokua unakua na kubadili interests. Hamtakiwi kulaumiana kwa kubadilika bali wote muendane mabadiliko yenu.
Mambo machache ya kujiridhisha ambayo huleta mitafaruku mikubwa na midogo baadaye nikama
1. Mtazamo wenu kwa pesa, je gender relationships kwenye swala la pesa liko vipi, mishahara mezani? Je shared accounts? Etc
2. Watoto, je ni wakiume, wa kike, wasipokuwapo? Kuadopt?
3. Imani, je zinawaongoza, kwa kiasi gani, open to changes?
4. Wazazi, ndugu, watoto wa kulea, kufikia kusomesha
5. Sex? Open to new ideas, strict?
6. What do you expect a wife/ husband to do for you?
Na kadhalika jaribu kuwa wazi na misimamo yako, na ujue misimamo yake, utajua tu kama utaweza kuiheshimu na kuihimili siku zote za maisha yako.
Then hata kama ni kesho mama ingia kwenye ndoa yako kwa matumaini.
Ndoa nzuri zipo tu, siku zote, na mbaya zipo tu, wewe ni kuchagua,
ukishaamua utapata amani.
Wewe ulishawahi kupata ki