Kuumwa kichwa sio ugonjwa ila ni dalili ya kuwa unaweza kuwa mgonjwa. Ili kukusaidia zaidi nakubaliana na hoja ya kumpeleka hospitali, ila angalia dalili nyingine kama kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, maumivu ya viungo kama mgongo, kuharisha....vyote vinasuggest malaria, typhoid (kama mwanamke Pregnancy???), lakini kama ni kizunguzungu na kichwa anaweza kuangalia blood pressure yake vilevile kwani inaweza kuwa ni mojawapo ya dalili ya hypertension. Vilevile inawezekana akawa ana stress na vitu kama hivyo, hivyo historia yake ya afya na social inaweza kusaidia. Mpatie paracetamol kama kichwa bado kinauma/homa na muende hospitali