Msaada Pls nahisi kuchanganyikiwa

Tuambie kwanza cha maan kilichopo kwenye mail yake ndefu. Put it differently anatoa sababu gani ya kimsingi kukupotezea na sasa imekuwaje anataka kurenew?
 
listen to your heart but dont let your heart control your mind......

kuwa na unayempenda , usiwe na mtu kwa sababu upo desparate unataka ndoa....
isije kuwa mwanaume wa kwanza huyo kagundua your happy na mtu mwingine anataka kukuvurugia.....
kuna baadhi ya watu wapo hivyo , akili kichwani mwako

na huyo ambaye bado anajijenga mnaweza jijenga pamoja...... mradi anakupenda na yupo serious.... akili mukichwa dada
 
Kuna muda historia huja na kuyaathiri maisha tunayoishi sasa lakini pia kuja kuishi maisha na mtu ambaye umemweka moyoni na mkayajenga pamoja maisha yenu kutoka kwenye shida mpaka raha ni kitu cha kusisimua sana!hivyo basi usiache historia ikayaathari maisha yako ya sasa sababu historia yenyewe ni ya maumivu ishi maisha yako ya furaha unayoishi sasa na pia kumbuka dini ni imani tu ya binadamu juu ya mwenyezi mungu na si usitengano wa binadamu wenye imani tofauti juu yake ila yote kwa yote upe moyo wako nafasi na mungu atakuongoza katika hilo
 


Wanaume ni noma, Kwa kucheza na hisia za w/ke. Yaani yule wa kwanza kavuruga thena kaaachia ngazi ukahamia kwa mwingine, tena una mpya umeamua kutulia unataka tena yule wa mwanzo arudi tena........Kweli mapenz yana run DUNIA.

Hebu tuambie unampenda yupi kati ya hao? au una cheki wapi kuna maslahi? je huyo aliyejijenga siku akiporomoka utakuja kumuacha urudi kwa huyu mpya?

Faham kuwa www una elimu yako na unaweza kujijenga zaidi ya m/me. Jiamini.........!

Tulia dada , tuliza mpira, focus on what you have.............!
 
Sasa kama huyo wa zamani wakati unakaa naye alishakwambia kwamba mko incompartible kwa mambo mengi wakati ukiwa naye,unategemea mtakuwa compartible kipindi hiki ambacho hamko pamoja?
 
Pole sana dada! Kwa ushauri wangu ni kuwa ANGALIA FUTURE YAKO! Sometym inabidi tuache tunachokipenda kwa maslahi ya kuandaa future nzuri ya ndoa na maisha kwa ujumla. Inabidi umchague ambaye unadhan mtafika mbali, mtakuwa na maisha mazuri, awe anakupenda nawe uwe unampenda. Je huyo ambaye mna dini tofauti yupo tayari kubadili dini? Au wewe upo tayari kubadili dini yako? Hujatuambia hilo. But kuwa makini ktk maamuzi utakayoyafanya.
 

Ukipitia comments zote hapo juu utakuwa umepata jibu...ila kumbuka mambo makuu..

Mapenzi ya kweli hayana dini; ....Mapenzi ya kweli hayana utajiri wa mali; .....Mapenzi ya kweli ni kujitoa muhanga kwa yule unayempenda.

Chukua tahadhali kubwa na huyo mpenzi wako wa zamani, angalia sana asije tawala fikra na maamuzi ya maisha yako. Ndugu na jamaa wa mpenzi wa zamani hawana sehemu kwenye maisha yako.
 
Ntaimalizia dear, nkipata ka muda. Well anadai alikua nayo but didn't work na anahisi mimi ndie sahihi kwake. Kwa vile kaandika mail sijaweza kumuuliza maswali kwa undani.
 
Follow ur heart ma dea,ur future is in ur hand!
 
Pole kwa kuchanganyikiwa bt to me naona hakuna sababu ya kuchanganyikiwa, moyo wako tu unatakiwa uamue uwe na nani kwa sababu hao wanaume wewe ndo unawajua kwa undani zaidi. Ushauri wangu kwako acha na huyo mwanaume wa kwanza, kama ni kujenga familia nadhani huyo wapi anafaa, suala la dini siku hizi siyo issue, wenye din moja wenyewe utakuta mmoja anaabudu kule mwingine huku ila muhamasishe tu muoane mapema asije akabadilika kama yule wa kwanza kama ni maisha mtajijenga pamoja
 
hata huyu wa pili sidhani kama unampenda kwa dhati maana ushaweka dini mbele, what i see ni kama unfil sorry for him. bado hujajijua unahitaji nini.
 
1.Uliyenae sasa ni wa dini tofauti, je swala la dini lina nafasi kubwa kwako?
2. Bado hajajijenga kimaisha, je unataka mteremko au upo tayari myajenge maisha kwa pamoja.
3: hana mpango wa kukuoa sasahv, je una haraka/uhitaji sana wa ndoa kwa sasa?
Jiulize maswali hayo na ukiona ndio ni nyingi kuliko hapana basi rudi kwa mpenzi wako wa zamani ila kama hapana ni nyingi kuliko ndio basi baki na uliyenae.
 
Olewa na uliye nae, huyo wa zamani kama alikuwa anatingisha kiberiti mwambie imekula kwake, mjibu kwa email na wewe
usionane nae, binadamu hasa sie wanawake tuna huruma sana hasa kwa wenzi wetu wa muda mrefu
 
Dada Mdhama, mimi nakushauri fanya ujanja mmoja...! Itisha kikao cha mashauri wewe na mtu yoyote ambaye unamwamini na ku-share mambo yenu ya karibu aidha rafiki au ndugu, kisha waite hao wapenzi wako, huyo wa zamani na huyo ulitenaye sasa.

Kisha wape hadithi yote ya maisha yako ya kimapenzi, kisha wasikilize watasema nini...!

Nina uhakika kabisa yule anayekupenda kwa dhati atajionyesha hapo. Na wewe unaweza kutoa uwamuzi wako mbele yao.
 
Olewa nna bwana wako wa zaman ukae unajutia maisha yako yote, Mungu keshakuonyesha sign kuwa huyo hkufai, kama ameweza kukuacha na kucheat wakati uko binti mbichi. itakuwa kukiwa kumekuchwa jua limezama, wakati huo ushazaa watoto watatu,kitu kimechoka...........embu tulia ulipopendwa wewe mtoto, usitange na dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…