Msaada Pls nahisi kuchanganyikiwa

Msaada Pls nahisi kuchanganyikiwa

Tuambie kwanza cha maan kilichopo kwenye mail yake ndefu. Put it differently anatoa sababu gani ya kimsingi kukupotezea na sasa imekuwaje anataka kurenew?
 
listen to your heart but dont let your heart control your mind......

kuwa na unayempenda , usiwe na mtu kwa sababu upo desparate unataka ndoa....
isije kuwa mwanaume wa kwanza huyo kagundua your happy na mtu mwingine anataka kukuvurugia.....
kuna baadhi ya watu wapo hivyo , akili kichwani mwako

na huyo ambaye bado anajijenga mnaweza jijenga pamoja...... mradi anakupenda na yupo serious.... akili mukichwa dada
 
Kuna muda historia huja na kuyaathiri maisha tunayoishi sasa lakini pia kuja kuishi maisha na mtu ambaye umemweka moyoni na mkayajenga pamoja maisha yenu kutoka kwenye shida mpaka raha ni kitu cha kusisimua sana!hivyo basi usiache historia ikayaathari maisha yako ya sasa sababu historia yenyewe ni ya maumivu ishi maisha yako ya furaha unayoishi sasa na pia kumbuka dini ni imani tu ya binadamu juu ya mwenyezi mungu na si usitengano wa binadamu wenye imani tofauti juu yake ila yote kwa yote upe moyo wako nafasi na mungu atakuongoza katika hilo
 
Nawasalimu wote kwa miyo wa dhati. Nina jambo ambalo linanisumbua sana nashare na ninyi mpate kunipa ushauri pls. Mimi ni binti wa makamo, nimeshamaliza chuo na nina kazi tayari. Kuna kaka mmoja ambaye tulisoma wote o level mkoa fulani then tukakutana Dar chuo fulani. Niseme wakati tukiwa chuo ndio tulikua karibu maana tulifanya course moja na tulikua karibu sana tukisaidiana kimasomo. Secondary tulikua darasa moja pia but hatukua karibu maana darasa lilikua na watu wengi kama mjuavyo shule za serikali, but chuoni ndo tuliweza ku interact. Wakati huo sikua na hisia zozote na yeye, niseme labda mawazo yangu siku focus kuwa na mahusiano naye, though yeye alitamani iwe hivyo na mara zote nilikua napinga, not that sikumpenda au labda nilikua na mtu mwingine no, i was just stubborn lol!

Well! Kwa ufupi baada ya chuo tuliendelea kuwasiliana though tulikua mikoa tofauti. Baadae niliendelea na masomo zaidi, na tuliendelea kuwasiliana. Baada ya masomo nikarudi mji/mkoa ambao yeye anaishi sasa, na well...tukawa wapenzi na kweli niseme tu ilifika kipindi nikamkubali na nikampenda kweli. But hali hailkua shari sana kwani alikua aki sema mara nyingi sana kwamba we are not compartible na mambo mengine mengi. Then, ikatokea akahamia mkoa mwingine kwa mambo ya kazi, na uhusiano wetu ukazorota sana. Nilijitahidi niwezavyo kuwasiliana naye though love ikawa inapotea pole pole. Nilijaribu kumtembelea huko alikohamia kikazi but hakunionyesha uchangamfu wala furaha. Nilimuuliza kama ana mtu mwingine, hakutaka kuwa muwazi so mi nilirudi kazini na hali ikawa mbaya zaidi ki mapenzi na hata mawasiliano. Niliteseaka kama mwaka mzima nika give up baada ya kuona simuelewi na hanielezi chochote cha maana.

So nipo kwenye mahusiano na mtu mwingine na nampenda naye ananipenda though tuko takika dini tofauti na sijui huko mbele itakuwaje though anaonyesha ishara zote kwamba yupo tayari kuwa na mimi in the future. Sasa yule jamaa wa zamani, bado tunawasiliana (sio kimapenzi,na sina tena feelings naye kabisa) kwa salamu tu na bahati mbaya au nzuri baadhi ya ndugu zake wananifahamu na tuna mahusiano mazuri tu, na wanadhani ndugu yao anampango na mimi labda wa kunioa. Sasa siku za karibuni ameniadikia email ndefu sana akijutia yote alofanya na anataka kunichumbia. Ki ukweli natamani ku settle, ila huyu nlio naye sasa bado anajijenga so sidhani kama tutaweza kuoana soon. Huyu wa zamani ana kila kitu (amejijenga kimaisha)na tupo dini moja. Ki ukweli nampenda sana huyu nlie naye sasa, na nogopa/ sithubutu hata kumuacha. Na kila mara ananiambia amefanya ujana sana, sasa ameamua kutulia na anadhani mimi ni mwanamke wake wa mwisho. Msaada please


Wanaume ni noma, Kwa kucheza na hisia za w/ke. Yaani yule wa kwanza kavuruga thena kaaachia ngazi ukahamia kwa mwingine, tena una mpya umeamua kutulia unataka tena yule wa mwanzo arudi tena........Kweli mapenz yana run DUNIA.

Hebu tuambie unampenda yupi kati ya hao? au una cheki wapi kuna maslahi? je huyo aliyejijenga siku akiporomoka utakuja kumuacha urudi kwa huyu mpya?

Faham kuwa www una elimu yako na unaweza kujijenga zaidi ya m/me. Jiamini.........!

Tulia dada , tuliza mpira, focus on what you have.............!
 
Sasa kama huyo wa zamani wakati unakaa naye alishakwambia kwamba mko incompartible kwa mambo mengi wakati ukiwa naye,unategemea mtakuwa compartible kipindi hiki ambacho hamko pamoja?
 
Pole sana dada! Kwa ushauri wangu ni kuwa ANGALIA FUTURE YAKO! Sometym inabidi tuache tunachokipenda kwa maslahi ya kuandaa future nzuri ya ndoa na maisha kwa ujumla. Inabidi umchague ambaye unadhan mtafika mbali, mtakuwa na maisha mazuri, awe anakupenda nawe uwe unampenda. Je huyo ambaye mna dini tofauti yupo tayari kubadili dini? Au wewe upo tayari kubadili dini yako? Hujatuambia hilo. But kuwa makini ktk maamuzi utakayoyafanya.
 
So nipo kwenye mahusiano na mtu mwingine na nampenda naye ananipenda though tuko takika dini tofauti na sijui huko mbele itakuwaje though anaonyesha ishara zote kwamba yupo tayari kuwa na mimi in the future. Sasa yule jamaa wa zamani, bado tunawasiliana (sio kimapenzi,na sina tena feelings naye kabisa) kwa salamu tu na bahati mbaya au nzuri baadhi ya ndugu zake wananifahamu na tuna mahusiano mazuri tu, na wanadhani ndugu yao anampango na mimi labda wa kunioa. Sasa siku za karibuni ameniadikia email ndefu sana akijutia yote alofanya na anataka kunichumbia. Ki ukweli natamani ku settle, ila huyu nlio naye sasa bado anajijenga so sidhani kama tutaweza kuoana soon. Huyu wa zamani ana kila kitu (amejijenga kimaisha)na tupo dini moja. Ki ukweli nampenda sana huyu nlie naye sasa, na nogopa/ sithubutu hata kumuacha. Na kila mara ananiambia amefanya ujana sana, sasa ameamua kutulia na anadhani mimi ni mwanamke wake wa mwisho. Msaada please

Ukipitia comments zote hapo juu utakuwa umepata jibu...ila kumbuka mambo makuu..

Mapenzi ya kweli hayana dini; ....Mapenzi ya kweli hayana utajiri wa mali; .....Mapenzi ya kweli ni kujitoa muhanga kwa yule unayempenda.

Chukua tahadhali kubwa na huyo mpenzi wako wa zamani, angalia sana asije tawala fikra na maamuzi ya maisha yako. Ndugu na jamaa wa mpenzi wa zamani hawana sehemu kwenye maisha yako.
 
Ntaimalizia dear, nkipata ka muda. Well anadai alikua nayo but didn't work na anahisi mimi ndie sahihi kwake. Kwa vile kaandika mail sijaweza kumuuliza maswali kwa undani.
 
Follow ur heart ma dea,ur future is in ur hand!
 
Pole kwa kuchanganyikiwa bt to me naona hakuna sababu ya kuchanganyikiwa, moyo wako tu unatakiwa uamue uwe na nani kwa sababu hao wanaume wewe ndo unawajua kwa undani zaidi. Ushauri wangu kwako acha na huyo mwanaume wa kwanza, kama ni kujenga familia nadhani huyo wapi anafaa, suala la dini siku hizi siyo issue, wenye din moja wenyewe utakuta mmoja anaabudu kule mwingine huku ila muhamasishe tu muoane mapema asije akabadilika kama yule wa kwanza kama ni maisha mtajijenga pamoja
 
hata huyu wa pili sidhani kama unampenda kwa dhati maana ushaweka dini mbele, what i see ni kama unfil sorry for him. bado hujajijua unahitaji nini.
 
1.Uliyenae sasa ni wa dini tofauti, je swala la dini lina nafasi kubwa kwako?
2. Bado hajajijenga kimaisha, je unataka mteremko au upo tayari myajenge maisha kwa pamoja.
3: hana mpango wa kukuoa sasahv, je una haraka/uhitaji sana wa ndoa kwa sasa?
Jiulize maswali hayo na ukiona ndio ni nyingi kuliko hapana basi rudi kwa mpenzi wako wa zamani ila kama hapana ni nyingi kuliko ndio basi baki na uliyenae.
 
Olewa na uliye nae, huyo wa zamani kama alikuwa anatingisha kiberiti mwambie imekula kwake, mjibu kwa email na wewe
usionane nae, binadamu hasa sie wanawake tuna huruma sana hasa kwa wenzi wetu wa muda mrefu
 
Nawasalimu wote kwa miyo wa dhati. Nina jambo ambalo linanisumbua sana nashare na ninyi mpate kunipa ushauri pls.... Kuna kaka mmoja ambaye tulisoma wote...

Well! Kwa ufupi ...tukawa wapenzi na kweli niseme tu ilifika kipindi nikamkubali na nikampenda kweli. ...alikua aki sema mara nyingi sana kwamba we are not compartible na mambo mengine mengi. ...love ikawa inapotea pole pole. Nilijaribu kumtembelea huko alikohamia kikazi but hakunionyesha uchangamfu wala furaha. ...Niliteseaka kama mwaka mzima nika give up baada ya kuona simuelewi na hanielezi chochote cha maana.

So nipo kwenye mahusiano na mtu mwingine na nampenda naye ananipenda though tuko takika dini tofauti na sijui huko mbele itakuwaje though anaonyesha ishara zote kwamba yupo tayari kuwa na mimi in the future. Sasa yule jamaa wa zamani, ...ameniadikia email ndefu sana akijutia yote alofanya na anataka kunichumbia. Ki ukweli natamani ku settle, ila huyu nlio naye sasa bado anajijenga so sidhani kama tutaweza kuoana soon. Huyu wa zamani ana kila kitu (amejijenga kimaisha)na tupo dini moja. Ki ukweli nampenda sana huyu nlie naye sasa, na nogopa/ sithubutu hata kumuacha. Na kila mara ananiambia amefanya ujana sana, sasa ameamua kutulia na anadhani mimi ni mwanamke wake wa mwisho. Msaada please
Dada Mdhama, mimi nakushauri fanya ujanja mmoja...! Itisha kikao cha mashauri wewe na mtu yoyote ambaye unamwamini na ku-share mambo yenu ya karibu aidha rafiki au ndugu, kisha waite hao wapenzi wako, huyo wa zamani na huyo ulitenaye sasa.

Kisha wape hadithi yote ya maisha yako ya kimapenzi, kisha wasikilize watasema nini...!

Nina uhakika kabisa yule anayekupenda kwa dhati atajionyesha hapo. Na wewe unaweza kutoa uwamuzi wako mbele yao.
 
Olewa nna bwana wako wa zaman ukae unajutia maisha yako yote, Mungu keshakuonyesha sign kuwa huyo hkufai, kama ameweza kukuacha na kucheat wakati uko binti mbichi. itakuwa kukiwa kumekuchwa jua limezama, wakati huo ushazaa watoto watatu,kitu kimechoka...........embu tulia ulipopendwa wewe mtoto, usitange na dunia
 
Back
Top Bottom