mdogo wangu anafunga ndoa mwezi wa tisa, tupo kwenye process ila jan amegundua mchumba wake ana mwanamke na mtoto mchanga wa miezi mmitatu wamefanana kama mapacha, alizaa naye akiwa arusha amemleta dar amempangia nyumba ila jamaa ni smart imetumika trick kali sana kumnasa, mdogo wangu amechanganyikiwa sana nimemwambia kila neno nmechoka, embu nipeni tips za kumsaidia, ndani hakupikwi wala hakuliki.
Dah! Mimi wakati mwingine huwa napata hasira kidogo just 0.0001% yaani kwa ufupi huwa nakereka ninaposoma nyuzi kama hizi. Huwa najiuliza hivi iki kizazi cha tovuti doti kom, huwa wanaishi dunia nyingine tofauti na hii tonayo ishi sisi au basi wanafanya makusudi tu au wanatafuta umaharufu kupitia mitandao...!?
Joyceline!? Nina maswali hapa kidogo ya kukuuliza.
Mosi wewe na mdogo wako mnaish dunia hii hii tunayoishi sisi wengine wote au mpo sayari ya Mars kama sio Pluto au Jupiter?
Pili kama jibu lako kuwa mpo satari yetu ya earth ambayo ndio dunia, hope mnaishi mitaani kwenye nyumba za kawaida kama si kijijini kama ilivyo desturi na si porini. Na ni matumaini kuwa mmezungukwa na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu kama si wazazi.
Je mmekwisha wasiliana na wazazi wenu kama si wa pande zote mbili na kuwasilisha duku duku lenu wewe na mdogo wako?
Hiyo ndoa ujasema itafungwa kwa imani ipi, je itakuwa ni ndoa ya kijadi (kimila), kidini au kiserikali. Vyovyote itakavyokuwa, ni desturi na utamaduni wetu sisi Waafrika kuwashirikisha wazazi kwa asilimia zote, wazazi, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na majilani.
Sasa kama wazazi wapo na wameshirikishwa kwenye mipango yote ya ndoa, tangia uchumba mpaka posa, mmeshindwa vipi kuwaona na kuwataka ushauri?
Je hamuwathamini wazee wenu?
Kama ni ndoa ya Kijadi, mnashindwa kuwaona wazee wa ukoo wenu au wa huyo mume mtarajiwa.
Kama ni ndoa ya kidini, kuna wanao husika kulingana na imani yenu.
Waoneni hao kwanza nilio wataja hapo juu, na nina matumaini makubwa kabisa mtapata msaada wenye kueleweka.