Msaada; Rafiki yangu vidole vyake na mdomo havichezi na mishipa ya kichwa inamuuma

ma-effect

Senior Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
100
Reaction score
137
Juzi jioni rafiki yangu alikunywa Konyagi. Kwa navyoujua unywaji wake, mi naona alikunywa kwa wastani. Tatizo limejitokeza jana.

Vidole vyake vilinata vikawa havichezi, mkono nao ukawa umeganda, mdomo akawa hawezi kuachama, akawa analalamika kuwa mishipa ya kichwa inamuuma sana, akawa anapumua kwa nguvu na kuongea kwa shida kisa haachami vzuri.

Nilimpeleka hospitali wakampima BP wakakuta iko kawaida, Sukari nayo ilikua kawaida. Baada ya kama lisaa hivi, vidole vikaanza react, akawa anaachama fresh.

Naomba niulize tatizo ilikua ni nini hasa?!! Au ni effect ya Konyagi aliyokunywa?! Na alimwambia daktari kuwa hajawahi pata ajali akaumiza kichwa.
 
Maji konyagi inakunywa maji,... Usinywe kwa pupa,
 
Poleni. Sijawahi kukutana na kesi kama hiyo katika pitapita zangu zote. Kwa hiyo kwa uzoefu wangu ninakuambia hilo tatizo halijasababishwa na konyagi, labda kinywaji alichokunywa haikuwa konyagi.
 
TIA (Transient Ischaemic Attack)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…