Msaada: Rangi ya gari inayovumilia jua la Dar!

Msaada: Rangi ya gari inayovumilia jua la Dar!

Hili jua la hapa mjini ni tatizo kubwa sana kuna fundi alimponda mwenzake kapiga vibaya nikampa yeye arudie chuma imeanza kupoteza ung'aavu tena, waliniambia shida ni chumvi maana napaki pembeni ya bahari ila naamini ni jua maana kila nikifungua gari wakati wa kuondokq inakua kama oven
 
Wakuu msaada kwenye tuta, gari nimeagiza hata miezi mitatu haijapita ila rangi inapauka kwa speed kali sana! Nilinunulia cover wakati inafika tu ila haijasaidia kitu. Ila cha ajabu nina jirani yangu gari yake hata haifuniniki ila haijapauka hata kidogo.

NB: Rangi ya gari ni blue, ila naweza badili kwenda nyingine itakayofaa!

Natanguliza shukrani
Kama bodi Haina shida nakushauri usipige rangi kwanza jaribu kuipiga polish inaweza ridi kwenye Hali yake vizuri tu boss
 
Kama bodi Haina shida nakushauri usipige rangi kwanza jaribu kuipiga polish inaweza ridi kwenye Hali yake vizuri tu boss

Poa mkuu basi nitajaribu hii kwanza
 
Hili jua la hapa mjini ni tatizo kubwa sana kuna fundi alimponda mwenzake kapiga vibaya nikampa yeye arudie chuma imeanza kupoteza ung'aavu tena, waliniambia shida ni chumvi maana napaki pembeni ya bahari ila naamini ni jua maana kila nikifungua gari wakati wa kuondokq inakua kama oven

Sema mafundi wanaaoponda wenzao mara nyingi wanakuwaga chenga!
Nimejaribu kufanya research google, wanapendekeza light color( white au silver), au rangi yeyote yenye metallic finishes!

Hilo ni jua linapiga direct, maana kwangu roof haitamaniki ila pembeni , bonnet na boot viko poa tu!
 
Back
Top Bottom