Mkuu hapa kuna mambo mengi.
Kwanza ni suala la uzoefu na masuala ya utafiti. Vyuo vikuu vyetu vingi wahadhiri wake wana masters tu. Wengi (si wote) wenye masters wamefanya utafiti na kuandika tasnifu(dissertation/thesis), lakin kimsingi, hata mwenye masters ni mwanafunzi wa utafiti, ni ngazi ya kujifunza utafiti. Kuna baadhi ya vyuo-hasa ulaya hawafanyi Research kwa ngazi ya masters bali Project na hivyo wanakosa msingi wa kufanya utafiti. Mtu mwenye PhD au profesa ndo anaaminika kwamba ameiva kwenye utafiti na mara nyingi unapofanya PhD unapata guidance ya kiufundi zaid kuliko ya utafiti. Kwa kifupi, wahadhiri wengi hawana uzoefu wa utafiti na hivyo hawezi kumsimamia mwanafunzi ipasavyo.
Pili, kuna suala la wanafunzi wenyewe kuwa wavivu na kutokuwa na msukumo na udadisi. Siku hizi mtu anafanya masters kwakuwa amemaliza bachelor lakin hajapata kazi, so anaunganisha. Uhalisia ni kwamba mtu inabidi afanye kazi kwanza ili kupata uzoefu na kugundua mambo mbalimbali akiwa kazin ambayo hakufundishwa chuo. Kwa namna hii, masters na mambo ya utafiti yanakuwa yanaenda vizuri kiasi. So kikubwa ni msukumo wa mwanafunzi mwenyewe, tena afadhali huyu anaomba msaada huu, wengine huwa wanatafuta pesa na watu wa kuwaandikia-ambayo ni mbaya zaidi.
Mwisho, nikubaliane nawe kwa kiasi fulani kwamba wanafunzi wanatakiwa wawe independent, waache kutafuta njia za mkato kama kuandikiwa kazi na kukopi kazi za wengine. Pia supervisors tuwasaidie wanafunzi tunaowasimamia kwa kusoma kazi zao kwa wakati na kutambua kwamba hao ni watu wanaojifunza hatua kwa hatua kufanya utafiti.