Msaada service ya mitsubishi Outlander 2007

Najua vipi kama gari ni CVT?
 
Uzi kama huu ni kawaida sana kuwakuta wamiliki wa Magari ya Kampuni ya Toyota waking'aza ng'aza tu macho kutokana na kukosa cha kuchangia.

Maana wenyewe wakienda gereji, huwa wanabadilishiwa oil na mazagazaga yoyote yale yatakayo ambiwa na mafundi. Yaani hakuna cha oil ya CVT wala nini.
 
Nipe namba yake nikuadd kwenye group la wamiliki wa outlander nchi nzima. Wanatoa ushauri kuhusu hilo gari pendwa. Tupo zaid ya 300

Fungua PM mkuu nikutumie namba, au please naomba unitumia PM
 
Nipe namba yake nikuadd kwenye group la wamiliki wa outlander nchi nzima. Wanatoa ushauri kuhusu hilo gari pendwa. Tupo zaid ya 300
Naomba link ya hilo group maana na mimi ni mmoja wao tafadhali
 
Tukianza na Engine Oil, recommend oil kulingana na Manufacturer ni 0W-20 with SN API indication. Lakini pia unaweza tumia 5W-30 kama mbadala kutokana na mazingira yetu lakini pia iwe na symbol ya SN

Engine Oil unaweza tumia PUMA, LIQUIMOLY, ATLANTIC, CASTROL & TOTAL ila uzipate kwenye vituo vyao vya mafuta au kwa trusted dealers


2. Kuhusu Gearbox Oil kwa model hio ya 2007, karibu zote zinatumia CVTF-J1 (Kama utafanya complete flush basi itakubidi uandae lita 7.8, ila kama unafanya normal drain and fill basi itakuwa around 5.6 lita (Ila wengi wanafanya kupima kiasi kinachotoka na kurudisha kiasi hicho hicho)
NOTE: Kuna upgrade ya CVTF-J1 ambayo ni CVTF-J4, hii ilitengenezwa kusolve issue ya overheating ambayo ilikuwa reported mara kwa mara kwenye gari za Mitsubishi zilizokuwa zinatumia CVTF-J1.......Hivyo unaweza pia kuitumia kama mbadala for improved performance and fuel economy.


Kingine kama utatumia CVTF-J4, Itakupeleka mpaka km 40,000 ndio ubadilishe gearbox oil nyingine


3. Transmission Oil una maanisha nini? maana gearbox oil ndio transmission oil yenyewe ila kama una maanisha Transfer Oil (Differential/rear axle) basi tumia HYPOID GEAR OIL API CLASSIFICATION GL-5 SAE 80 au 90 cheki hapo juu kwenye specifications.

4. Kuhusu STEERING FLUID hapo recommended ni ATF DEXRON III au DEXRON II


Enjoy Mitsubishi Outlander brother.
Kama una swali jingine uliza.
 
Umenena vyema nami nimepokea elimu hapa.
 
.Hongera kwa kuzingatia services ukishajua oil gani zitumike nenda kwa authorized dealer au vituo vya mafuta kama total oryx na puma nunua oil mwenyewe...mafundi wengine si waaminifu watakuwekea oil ya bei chee na chini ya kiwango ili apige hela
Kuna Fundi ambae nimeikuta kununua Dumu la Lt 20 la oil engine nahisi ilikuwa SAE 40. Kuna wateja wanaleta gari/ wanampigia akachukue gari lilipo na kulileta ofisini kwake. Anachukua Ile oil anaiweka kwenye Dumu la Lt 4 au Tano anaiweka kwenye gari, then mteja anaonyeshwa Lile Dumu analipa anasepa. Ukimwambia nataka 10W30 anatafuta Dumu la hivyo. Wateja wengi hawakagui so yy haweki seal.
Kwa mtindo huu akifanya hivi kwenye haya magari ya kisasa ni kilio....

NB. Tuwe makini hasa na mafundi tunaowaamini. Usipende kumwachia yy anunue Kila kitu kama hakuna ulazima.
 
kama ndio service ya kwanza au ndio gar la kwanza ni bora kuangalia fundi mwaminifu au garage kubwa inayofahamika kubari kutoboka mfuko ili wakufanyie service inayoeleweka na kwa uaminifu mda huo unaangalia wa bei nafuu ambae anaweza kufanya service na repairs kwa affordable price bila kona nyingi

kufanya service inajumuisha mambo mengi sana sio kubadili tu fluids, filters, na pumps ni zaidi ya hapo.
 
🫡
 
Mkuu samahani njoo hapa unipe ushauri ila usinisimange 🤣🤣 nimenunua Brevis linatembea ile mbaya ila naomba kujua ni oil gani nzuri kwa injini hii 1JZ FSE na inawekwa Lita ngapi na transmission oil pia niweke ipi na ni lita ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…