telex
JF-Expert Member
- Apr 26, 2015
- 406
- 103
Wadau, nina mdogo wangu wa kiume ambaye yupo kidato cha nne sasa, juzi nilipewa taarifa kutoka shuleni kuwa amekamatwa na polisi na kuwekwa ndani, nilipofuatilia shuleni nikaelezwa kuwa mdogo wangu huyo amekamatwa kutokana na kumpa mimba binti wa kidato cha pili katika shule hiyo hiyo na binti huyo amepelekwa hospitali na kajifungua tayari.
Baada ya hapo nikawatafuta wazazi wa binti ili tuzungumze juu ya tatizo hili, nikafanikiwa kuwapata na tukazungumza ila utata uliojitokeza ni hivi;
Wazazi wa binti wanataka walipwe milioni tatu na laki sita kama gharama za ada waliyoipoteza kwa binti yao na faini kwa tatizo lililotokea, tulikubaliana nao ila tukawaambia kwa kuwa ni ghafla sana watupe mda wa kutafuta hizo fedha, kitu hiki wazazi wa binti hawakubaliani nacho hata kidogo. Wanataka walipwe leo leo la sivyo tuende mahakamani haki ikatendeke.
Wadau naomba msaada wa kisheria juu ya hili kwani ukizingatia hawa wote ni wanafunzi.
Nawasilisha