Msaada: Sheria inasemaje wanafunzi wakipeana mimba?

Msaada: Sheria inasemaje wanafunzi wakipeana mimba?

telex

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2015
Posts
406
Reaction score
103
Wadau, nina mdogo wangu wa kiume ambaye yupo kidato cha nne sasa, juzi nilipewa taarifa kutoka shuleni kuwa amekamatwa na polisi na kuwekwa ndani, nilipofuatilia shuleni nikaelezwa kuwa mdogo wangu huyo amekamatwa kutokana na kumpa mimba binti wa kidato cha pili katika shule hiyo hiyo na binti huyo amepelekwa hospitali na kajifungua tayari.

Baada ya hapo nikawatafuta wazazi wa binti ili tuzungumze juu ya tatizo hili, nikafanikiwa kuwapata na tukazungumza ila utata uliojitokeza ni hivi;

Wazazi wa binti wanataka walipwe milioni tatu na laki sita kama gharama za ada waliyoipoteza kwa binti yao na faini kwa tatizo lililotokea, tulikubaliana nao ila tukawaambia kwa kuwa ni ghafla sana watupe mda wa kutafuta hizo fedha, kitu hiki wazazi wa binti hawakubaliani nacho hata kidogo. Wanataka walipwe leo leo la sivyo tuende mahakamani haki ikatendeke.

Wadau naomba msaada wa kisheria juu ya hili kwani ukizingatia hawa wote ni wanafunzi.

Nawasilisha
 
Hao wazazi wamepata pa kutokea...kuzaa binti ni saccos kumbe? Mkitoa hiyo hela itakuwa mahari? Vipi mtamchukua binti moja kwa moja ama?
 
Kama bint yupo chini ya miaka 18 huko ni kubaka na ikithibitika ni Kuala 30 jela, mtenda kosa umri wake haujalishi km yupo chini ya miaka 18, sheria inatoa msamaha KWA mtenda kosa km atakuwa chini ya more aka 12. Nenda uongee nao tena muyamalize, tofauti nahivyo ikithibitika mahakamani, utampoteza Dogo.

Kingine swala LA hiyo hela eti ni gharama za Ada ndo ulipe wewe, kisheria hilo swala halipo, labda KWA kuwa wamepata sehem yakukukamatia
 
Back
Top Bottom