Msaada, sheria ya umilikaji wa viwanja/ardhi.

Msaada, sheria ya umilikaji wa viwanja/ardhi.

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,986
Reaction score
5,058
Kuna maeneo ni mashamba ambayo yanalimwa na wazazi wetu. Halmashauri wanataka kuuza viwanja eneo hilo na wanasema hatupati chochote, je sheria ya ardhi inasemaje? Hatuna haki ya kumiliki viwanja eneo hili kwa kulipia gharama za upimaji? Inaruhusiwa halmashauri kupima eneo bila kuwasiliana na wamiliki wa kimila(traditional owners). Haya ni maeneo ambayo yamemilikiwa na babu zetu kabla hata halmashauri haijaanzishwa. Hata zilipojengwa ofisi za halmashauri walipewa na babu zetu eneo kwa wakati huo.
 
Duh! Wanasheria wetu wako bize na kesi ya lwakatare! Ngoja niendelee kusubiri.
 
Ebana kwa kifupi ninyi mnamiliki hiyo ardhi kwa kitu kinaittwa customary right of occupancy..sababu ardhi yenu haijapimwa..kwahiyo unaweza ukafanya utaratibu mkaipima hiyo ardhi then mkapata granted right of occcupancy ambayo ni certificate ya umiliki ardhi iliyopimwa..land act ya mwaka 1999 re 2002 hiyo hati ya umiliki wa kimila na hiyo ya granted ziko sawa kwahyo hao watendaji wasikutishe kitu..kama watauza lazima ulipwe fidia kutokana na ulivyondeleza hiiyo sehemu.over...
 
Back
Top Bottom