Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,986
- 5,058
Kuna maeneo ni mashamba ambayo yanalimwa na wazazi wetu. Halmashauri wanataka kuuza viwanja eneo hilo na wanasema hatupati chochote, je sheria ya ardhi inasemaje? Hatuna haki ya kumiliki viwanja eneo hili kwa kulipia gharama za upimaji? Inaruhusiwa halmashauri kupima eneo bila kuwasiliana na wamiliki wa kimila(traditional owners). Haya ni maeneo ambayo yamemilikiwa na babu zetu kabla hata halmashauri haijaanzishwa. Hata zilipojengwa ofisi za halmashauri walipewa na babu zetu eneo kwa wakati huo.