**Msaada shule ya sekondari KIBAHA BOYS**

**Msaada shule ya sekondari KIBAHA BOYS**

daby mouser

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2012
Posts
206
Reaction score
73
Hiv hii shule kimazingira ya kiufundishaj kuanzia uwepo wa waalim,na nyenzo zingine za ufundishaj ziko vip??na vip kuhusu mazingira yana ushawish?na maisha ya pale kwa ujumla?nimechaguliwa hapo A LEVEL PCB naomben ushauri wenu!!ila bado sijareport coz of sam matatizo hiv ambayo bado napambana nayo nimeshatuma EXCUSE na wamekubali kunipa mda kidogo wa kureport!

ANGALIZO:KAMA HUNA CHCHOTE CHA KUCHANGIA BETTER UIACHE HII THREAD KAMA ILIVYO USTAARAB WA KUELIMISHAMANA PLUS MATURITY NDO NYENZO MUHIM ZINAZOHITAJIKA KWENYE HII THREAD!
 
Sasa wewe dogo unachokitaka nini? Kibaha matokeo yake huyajui? Hata kama hakuna walimu ila ushirikiano walio nao wanafunzi unatosheleza kabisa kwa mwanafunzi kufanya vizuri. Kwa ufupi ukipata div iv basi utajulikana shule nzima maana unaweza kuwa peke yako.

Kwa kumalizia nakupa ongera kwa kuchaguliwa kidato cha tano ila safari ndio inaanza juu ya mustakabari wa maisha yako ya elimu ya juu (university). Hapo ndio pakusomea boom (loan), course ya ukweli na kadhalika.
 
Hiv hii shule kimazingira ya kiufundishaj kuanzia uwepo wa waalim,na nyenzo zingine za uundishaj ziko vip??na vip kuhusu mazingira yana ushawish?na maisha ya pale kwa ujumla?nimechaguliwa hapo A LEVEL PCB naomben ushauri wenu!!ila bado sijareport nishatuma excuse na wameikubali!

Mpumbavu sana wewe kiduku gen.
Sasa unauliza mazingira wakati umeshakataa kwenda hiyo shule? Nimesoma pale miaka minne, ila kwa upuuzi huu siwezi kupoteza muda kukuelezea mazingira. Mwaka 2014 ukishafeli kwenye hiyo private schule unayotaka kwenda ndo unitafute nikuambie ulikokosea...
 
Sasa wewe dogo unachokitaka nini? Kibaha matokeo yake huyajui? Hata kama hakuna walimu ila ushirikiano walio nao wanafunzi unatosheleza kabisa kwa mwanafunzi kufanya vizuri. Kwa ufupi ukipata div iv basi utajulikana shule nzima maana unaweza kuwa peke yako.

Kwa kumalizia nakupa ongera kwa kuchaguliwa kidato cha tano ila safari ndio inaanza juu ya mustakabari wa maisha yako ya elimu ya juu (university). Hapo ndio pakusomea boom (loan), course ya ukweli na kadhalika.

shukran sana nimekupata!
 
sasa wew dhihaki ya nini jiheshim bas!,nimekuomba ushaur hayo mengine ya sijui mpumbavu yametoka wapi,mbona ukuaji wako hautumii vilivyo?,ningekuona mstaarab sana kama usingechangia chochote na kupita ukaenda zako!MARA NYINGINE JARIB KUTUMIA HATA AKILI YA KUZALIWA KAMA YA DARASAN HAIKUSAIDII!hadhi y kusema kama umesoma kibaha huitendei haki kabisa!huna SONI YA USTAARAB!then hizo mambo za sijui shule ya private sijui umezitoa wapi,hivi umeisoma status niliyo update hapo juu??UFAHAM ni kitu tunacho fundishwa kabla hatujaanza kusoma lugha yoyote ili kupima uelewa(uchanganuo) wetu wa kitu tunachosoma,ningekushauri urudi hapo juu,then ndo uanze kuflow shits zako!!Angalizo tu!
 
Ndugu yangu, katika moja ya shule bora tanzania hapa huwezi kuiweka kibaha pembeni hata, nimemaliza PCM pale 2002, na intake yetu tulikuwa watatu kitaifa kimatokeo.... Ingawa inaitwa/ilikuwa inaitwa special school lakini naomba nikuonye kuwa uspeciality pale si kutafuniwa kila kitu.... unahitaji muda mwingi wa kujisomea na hasa kinachowafanya watu wafaulu ni kuwa kuna ushindaji mkubwa sana kati yao, watu wanashindana na wana ile hali sikubali fulani anipite...kuna wakati hawalali, wanasoma 24/7... so wakati mwingine uspecial si kwamba unajua saanaaa au una kipaji kikubwaaa inapokuja kwenye hizi special school..

Sijajua enzi hizi ila enzi za mwampaja..wakuu watakumbuka kuwa ilikuwa full kuku, yani ilikuwa raha tu..msosi ulikuwa mzuri usipime, nimesoma O-level tabora boys, ila chakula kibaha ilikuwa juu mara dufu..Walimu wapo na wanajitahidi, ila si kwamba watakufundisha kama unaanza chekeckea NO... wanakutengenezea njia na itabidi usome kujiendeleza!! Mitihani internal ni migumu balaa utasema afadhali NECTA... but inakufanya mtu ujione hujui na uongeze juhudi... but at last tulimaliza shule vizuri sana na tulikuwa na division one karibu 70, na three zilikuwa mbili au tatu tu, tena mbili za penalty kama sikosei
So please nenda maana mnakutana mafahali wengi, na unajua mafahali ni ushindani na kwa ushindani unajitengenezea njia ya kufaulu vzr... kama hutaki nenda kale mayai st. Marys
 
Hiv hii shule kimazingira ya kiufundishaj kuanzia uwepo wa waalim,na nyenzo zingine za ufundishaj ziko vip??na vip kuhusu mazingira yana ushawish?na maisha ya pale kwa ujumla?nimechaguliwa hapo A LEVEL PCB naomben ushauri wenu!!ila bado sijareport coz of sam matatizo hiv ambayo bado napambana nayo nimeshatuma EXCUSE na wamekubali kunipa mda kidogo wa kureport!

ANGALIZO:KAMA HUNA CHCHOTE CHA KUCHANGIA BETTER UIACHE HII THREAD KAMA ILIVYO USTAARAB WA KUELIMISHAMANA PLUS MATURITY NDO NYENZO MUHIM ZINAZOHITAJIKA KWENYE HII THREAD!
Kijana wangu, mm nimemaliza A level (CBA, kabla ya kuleta hiyo PCB) hapo na nilipata Div. I, hakika sijaona shule yenye mazingira mazuri ya kusoma kama hiyo, tatizo lenu vijana mnapenda sana kuchagua shule, tatizo sio shule bali ni mwanafunzi mwenyewe. Anyway, kwa ushauri zaidi Rejea pia post ya Sangito.
 
Hizi fake ID's zetu zinaficha mengi sana aisee,Kumbe JF wamejaa watoto wengi sana eeenh??Hebu nenda kasome wewe dogo acha mbwembwe!!
 
Katika shule za serikali zenye mazingra mazur ya kupigia msuli,kibaha inaongoza,pia wanapga msoc mzuri tofaut na lishule kama pugu,so we dogo nakushaur uende pale,ila kumbuka ukienda pale kula na kufanya anasa,lazma mama ndalichako akule kichwa hyo 2014,ila ukienda kupga shule bac tunategemea utakua tanzania one hyo 2014.over
 
Nisalimie wakazi wa Skandia na Kibo. Enzi zangu hapo ni 1972-73. Palikuwa first class. Kijiji cha mfano (model village) chini ya Waskandinavia. Unashangaa? Ulikuwa hujazaliwa?
 
songíto;3713276 said:
ndugu yangu, katika moja ya shule bora tanzania hapa huwezi kuiweka kibaha pembeni hata, nimemaliza pcm pale 2002, na intake yetu tulikuwa watatu kitaifa kimatokeo.... Ingawa inaitwa/ilikuwa inaitwa special school lakini naomba nikuonye kuwa uspeciality pale si kutafuniwa kila kitu.... Unahitaji muda mwingi wa kujisomea na hasa kinachowafanya watu wafaulu ni kuwa kuna ushindaji mkubwa sana kati yao, watu wanashindana na wana ile hali sikubali fulani anipite...kuna wakati hawalali, wanasoma 24/7... So wakati mwingine uspecial si kwamba unajua saanaaa au una kipaji kikubwaaa inapokuja kwenye hizi special school..

Sijajua enzi hizi ila enzi za mwampaja..wakuu watakumbuka kuwa ilikuwa full kuku, yani ilikuwa raha tu..msosi ulikuwa mzuri usipime, nimesoma o-level tabora boys, ila chakula kibaha ilikuwa juu mara dufu..walimu wapo na wanajitahidi, ila si kwamba watakufundisha kama unaanza chekeckea no... Wanakutengenezea njia na itabidi usome kujiendeleza!! Mitihani internal ni migumu balaa utasema afadhali necta... But inakufanya mtu ujione hujui na uongeze juhudi... But at last tulimaliza shule vizuri sana na tulikuwa na division one karibu 70, na three zilikuwa mbili au tatu tu, tena mbili za penalty kama sikosei
so please nenda maana mnakutana mafahali wengi, na unajua mafahali ni ushindani na kwa ushindani unajitengenezea njia ya kufaulu vzr... Kama hutaki nenda kale mayai st. Marys

dah mkuu shukrani sana bradha nimekusoma kwa marefu na mapana,uchanganuzi wako umenifanya nipate mengi ambayo sikuwah kufikiria kuyapata akhsante na mungu akuzidishie roho ya ukarim uliyonayo,tupo pamoja!!
 
Hizi fake ID's zetu zinaficha mengi sana aisee,Kumbe JF wamejaa watoto wengi sana eeenh??Hebu nenda kasome wewe dogo acha mbwembwe!!

hehehe usijal kaka,hata mbuyu ulianza kama mchicha,kitabu ndicho tulichoagizwa so kitakamuliwa to the MAXIMUM!
 
Katika shule za serikali zenye mazingra mazur ya kupigia msuli,kibaha inaongoza,pia wanapga msoc mzuri tofaut na lishule kama pugu,so we dogo nakushaur uende pale,ila kumbuka ukienda pale kula na kufanya anasa,lazma mama ndalichako akule kichwa hyo 2014,ila ukienda kupga shule bac tunategemea utakua tanzania one hyo 2014.over

hahaha usijal brother tutalikamilisha hilo hata kwa kusoma kwa mwanga wa njiti ya kibiriti...sitafanya makosa akhsante sana kwa hamasa yako!ONE HEART!
 
Nisalimie wakazi wa Skandia na Kibo. Enzi zangu hapo ni 1972-73. Palikuwa first class. Kijiji cha mfano (model village) chini ya Waskandinavia. Unashangaa? Ulikuwa hujazaliwa?

haahaha kwel nilikuwa sijazaliwa bado usijal ntawafikishia haha!TUPO PAMOJA!!
 
Dogo Kibaha haimtupi mja wake.

Tulikuwepo pale hadi 2009 A level,nenda ukasome then ukimaliza uje chuo tusome ,sawa!
 
Mshukuru MUNGU kwa kuchaguliwa katika shule nzuri kama ile! Pale ukifeli ni bahati mbaya au ulipenda. Mazingira ni mazuri mno!
Ukifika kamsalimie Kashinde na ukae bweni la Skandia kwani ni karibu na facilities zote!
Hongera mdogo wangu
 
Sasa wewe dogo unachokitaka nini? Kibaha matokeo yake huyajui? Hata kama hakuna walimu ila ushirikiano walio nao wanafunzi unatosheleza kabisa kwa mwanafunzi kufanya vizuri. Kwa ufupi ukipata div iv basi utajulikana shule nzima maana unaweza kuwa peke yako.

Kwa kumalizia nakupa ongera kwa kuchaguliwa kidato cha tano ila safari ndio inaanza juu ya mustakabari wa maisha yako ya elimu ya juu (university). Hapo ndio pakusomea boom (loan), course ya ukweli na kadhalika.

Wakati wa enzi zetu hapo, kulikuwa na paper kila jumatatu alafu matokeo yanawekwa hadharani kwenye ubao uliondani ya kioo kilichofunikwa na nyavu za chuma. Mtu wa kwanza alikuwa anaanza na 35, watu walikuwa wanataga kila kukicha lakini mwisho wa yote darasa zima tulipata Division One. Nakushauri KB ni pazuri kimazingira, kimasomo, kijamii, kimichezo, wakati wetu tulikuwa tunakula kuku na mayai yake mpaka. Ni shule ambayo inakufanya uwe mwenye kujiamini na kujitegemea, kama ni mwanafunzi uliyezoea spoon feeds usiende.
 
Maktaba ya mkoa ipo hapo chuo kikuu huria kipo hapo shule ya sekondari tumbi ipo hapo chuo cha uganga kipo hapo fdc kipo hapo hospital ya tumbi ipo hapo shule ya secondari kibaha wasichana ipo hapo shule ya msingi tumbi ipo hapo shamba la ngombe na kuku. Sema unataka nini sasa
 
Back
Top Bottom