Wakati wa enzi zetu hapo, kulikuwa na paper kila jumatatu alafu matokeo yanawekwa hadharani kwenye ubao uliondani ya kioo kilichofunikwa na nyavu za chuma. Mtu wa kwanza alikuwa anaanza na 35, watu walikuwa wanataga kila kukicha lakini mwisho wa yote darasa zima tulipata Division One. Nakushauri KB ni pazuri kimazingira, kimasomo, kijamii, kimichezo, wakati wetu tulikuwa tunakula kuku na mayai yake mpaka. Ni shule ambayo inakufanya uwe mwenye kujiamini na kujitegemea, kama ni mwanafunzi uliyezoea spoon feeds usiende.