Msaada: Sikio langu limeziba

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Habari wataalam wa afya.
Sikio langu lilikua linawasha kwa muda mrefu na kutoa nta za langu tofauti na kawaida (zinaelekea na rangi ya usawa)
Leo nilifanikiwa kumpeleka binti yangu hospital nikataka nami nilachunguze lakini bahati mbaya sikufanikiwa.
Niliporudi nyumbani sikio likaziba ghafla,kuona hivyo nikajaribu kuchokonoa kwa toothpick,nikatoa rundo la nta zilizoganda zenye harufu mbaya.Zilikua nyingi sana,sikio likazibuka kidogo tu badae likazipa tena.Nilijaribu kuweka maji kwa sindano lakini sikufanikiwa japo likazibuka kidogo na kuanza kusikia kwa mbali.
Naomba msaada nifanyaje aise linawasha sana kwa sasa na ndani limekua jekundu
 
Siku nyingine usitie hiyo toothpick zitakutoboa hilo sikio lako kisha unaweza kuwa wewe ni kiziwi. Chukuwa maji ya Uvuguvugu tia ndani ya sikio lako kisha uiname na huku unaliziba kwa kiganja chako cha mkono na huku unaziba na kufunguwa maji yakitoka litazibuka na uende Hospitali kutoa uchafu uliosababisha kuziba kwa sikio lako.
 

Asante mzizi mkavu,ndio natoka hospital masikio yote yamesafishwa...yalikua na uchafu mwingi sana (nta).Of course Dr amenishauri nistumie pamba wala toothpick tena,sababu naweza toboa sikio
 
Asante mzizi mkavu,ndio natoka hospital masikio yote yamesafishwa...yalikua na uchafu mwingi sana (nta).Of course Dr amenishauri nistumie pamba wala toothpick tena,sababu naweza toboa sikio
Asante kwa kuleta mrejesho ingawa nilikuwa sijauona siku zimepita kidogo lakini ninashukuru kwa kueleta feedback ubarikiwe Mkuu.Umefanya jambo la uungwana mkubwa kuleta feedback ingawa ni watu wachache wenye tabia kama yako hiyo.😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…