hii imenitokea wiki iliyopita, nmeshtuka saa 9 usiku nikakuta delivery report kwa mtu ambae hata sikuwa na mawasiliano nae mda mrefu sana, nikaenda kwenye sent sms sikuona kama kuna sms niliyotuma kabla, nikapotezea.
Nmewahi shuhudia hili tena nikiwa natumia TTCL, nilikua natafutwa na watu namba ngeni wanalalamika nmewatumia sms zisizoeleweka, nikiangalia kwenye simu sioni jumbe (hii sana sana ilikua inatokea mwisho wa mwezi). Kuna siku niliomba mtu anitumie screenshot n kweli na niliona codes ambazo sikutambua zina maanisha nini.