Msaada: Simu kutuma sms bila command

Msaada: Simu kutuma sms bila command

Cattigo

Senior Member
Joined
Nov 12, 2016
Posts
193
Reaction score
393
Wadau salamu kwenu.

Naomba ufafanuzi kwa wanaojua;

Natumia SAMSUNG A52 na Samsung A3 core. Kuna nyakati simu imetulia tu huitumii unaona inatoa pop-up notification kwamba "Sending sms"! Hii maana yake ni nini?

Ni simu ziko hacked au ndo inatuma zile diagnostic informations?

Any hint wakuu.

Asanteni.

~ C~
 
Hahaa hio sms inakuaje?
Anayetumiwa unamjua?
Anapata hio msg.

Kwa ufupi kuna maswali mengi
 
hii imenitokea wiki iliyopita, nmeshtuka saa 9 usiku nikakuta delivery report kwa mtu ambae hata sikuwa na mawasiliano nae mda mrefu sana, nikaenda kwenye sent sms sikuona kama kuna sms niliyotuma kabla, nikapotezea.

Nmewahi shuhudia hili tena nikiwa natumia TTCL, nilikua natafutwa na watu namba ngeni wanalalamika nmewatumia sms zisizoeleweka, nikiangalia kwenye simu sioni jumbe (hii sana sana ilikua inatokea mwisho wa mwezi). Kuna siku niliomba mtu anitumie screenshot n kweli na niliona codes ambazo sikutambua zina maanisha nini.
 
Tofauti na mimi ni kwamba hakuna cha delivery note wala sent sms inabakia!
 
Wadau salamu kwenu.

Naomba ufafanuzi kwa wanaojua;

Natumia SAMSUNG A52 na Samsung A3 core. Kuna nyakati simu imetulia tu huitumii unaona inatoa pop-up notification kwamba "Sending sms"! Hii maana yake ni nini?

Ni simu ziko hacked au ndo inatuma zile diagnostic informations?

Any hint wakuu.

Asanteni.

~ C~
Kama haijarogwa basi ina wazimu na kama haina wazimu basi ina pepo na kama haina yote hayo basi imechanganyikiwa
 
Jaman mim Nina Aquos Sense 5G shida yake nikituma sms Moja mpokeaji ana pokea sms 3

Msaada
 
Kuna uwezekano mtu kainstall kitu kinatuma SMS tazama hizo permission kama walivyokwambia au reset simu.
 
Nime reset Kila kitu lakin Bado yaan unatuma sms Moja ila kwa mpokeaj anapokea 3
 
Back
Top Bottom