Mm kwa nyongeza, jitahid Sana kupata mafundi wazur wa hiyo altenetor.
Mm nimewahi kupata shida Kama yako, na tatizo kweli ilikuwa altenetor lakin kwa bahat mbaya nilijikuta namaliza hela kutengeneza hiyo kitu.
Fund wa kwanza alisema tufungue altenetor tuangalie ndan. Baada ya kufungua akasema tatizo ni blash tuzisafishe. Akafanya hivyo kwa siku mbili tatizo likaisha. Akala hela
Baada ya muda mfupi, tatizo likarudia, nikampa fundi mwingine. Akasema hii ni altenetor mzee tufungue tuangalie ndani. Baada ya kufungua akasema altenetor imekufa kifaa kinaitwa cata out, akanionyesha, nikaenda kununua dukan 45,000 helf. Tukafunga tatizo likaisha. Baada wk taa ya betey ikawaka Tena.
Nilipo ona hivyo nikapeleka gari kwenye gereji ya wachina wapime kabisaa. Wakakuta Kuna kitu katika mfumo wa umeme kinachosababisha kuharibu altenetor.
Wakatengeneza, na mm pia kwa hasira nikanunua altenetor mpya na tatizo halikurudi.
So kwa maoni yangu mm nashauri Kama walivyo sema wakuu wengine kwamba uenda ni altenetor, Basi jitahidi upate fundi mzuri atakae weza kutoa sababu Kama ni altenetor kwann iharibike????
Hapa na mahanisha upate fund wa kukufanyia full scan ya umeme wote. Hawa wengine wa gereji bubu ni pasua kichwa. Yaan utafikir ni Mahita vs P.G.O