Msaada: taa ya Check engine inawaka

nenda kwa fundi! ila jua kuwa hakunaga passo nzima duniani, zote ni majanga! mwisho kabisa, we dume zima unaendeshaje ka passo?
Unataka nifanye biashara ya tax na Harrier ndugu yangu,mi hii ni gari ya biashara kwa ajiri ya consumption ya mafuta,tusikariri jamani,kwamba hili la kike au hili la kiume,....kuna sifa za kijinga unaendesha gari ya gharama lakini kulihudumia huwezi,ukipata safari ya Dar to Moro tu hapo unajifikiria,nina rafiki yangu ameninua Harrier lakini limekua kama pambo anaishia kupiga nalo picha,kulihudumia hawezi kila siku analia lia njaa!
 
Ujue sometimes hiz mambo ya sensors au haya magari ya kisasa ni kama simu tu.
Saa nyingine simu iki stack una restart na ikirudi mpya. Hivo hivo kwenye haya magari ya sasa hivi.
Chomoa terminal kwa muda flani unakuta mambo ya nakaa sawa.
Kichwa kikikuuma haimanisha kinataka dawa au umuone doctor. Labda umelala vibaya ama hunywi maji ya kutosha. Vitu vingine unamaliza mwenyewe tu mkuu.
 
nenda kwa fundi! ila jua kuwa hakunaga passo nzima duniani, zote ni majanga! mwisho kabisa, we dume zima unaendeshaje ka passo?
Mkuu ujuaje kama ni dume ! sijaona alikotaja jinsia yake
 
Mimi Nina Rav4 Mayai inawaka hiyo taa mwaka wa 4 sasa lakini hakuna tatizo lolote
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
tatizo lipo bosi ila hujaamua kulifuatilia...kafanye diagnosis utajua shida ikowapi...nikuulize swali..ulaji wa mafuta haujaongezeka kwa kiasi fulani???
 
Mimi Nina Rav4 Mayai inawaka hiyo taa mwaka wa 4 sasa lakini hakuna tatizo lolote
Dah mkuu, kama unaipenda hiyo gari ipeleke kwenye garage zenye mafundi wazuri. Isije ikakuharibia kitu kikubwa!
 
Kwanza kabisa kama taa unayomaanisha ni hiyo ya njano that's not check engine indicator, check engine ni red na iko kama birika

Pili kama check engine (kwa maana ya hiyo niliyotaja juu) ndio inayowaka, kitu cha kwanza angalia oil level, kama oil level iko low hiyo ndio sababu. Kinachofata ni kujua kwa nini oil imepungua, hapo unaweza kuhitaji fundi lakini possible reasons ni leakages (external or internal)

All the best
 
point of correction..
Hiyo taa unayosema ipo kama birika na inawaka nyekundu si check engine...hiyo ni taa ya oil pressure na haiwaki kwa sababu oil imezidi au imepungua..

yaa hiyo ya oil presure inawaka endapo pump ya oil haiwezi kusukuma oil ipande juu kwenye sehemu za engine....na taa hii ya oil ikiwaka ni hatari sana zima gari na ulivute mpaka garage.

Hiyo taa ya orange inayoonekana kwenye picha ndiyo chek engine ikiashiria kuna kitu kwenye engine kina hitilafu....hivyo kwa ushauri mwenue gari akafanye diagnosis ili kubaini tatizo.
 
Point of correction! Uko sahihi, ukiona gari inawaka taa ya check engine tambua kuanzia hapo vitu vitatu vinatokea.
1: imeongeza ulaji Mafuta
2: imeongeza moshi (huuoni)
3: inamiss (huihisi)
Na wakati mwingine hakuna chochote kati ya hivyo na wala hakuna tatizo lolote kwenye mfumo isipokuwa tu ni sensor yenyewe ndo imekufa.

Sensor inayohusika kuleta taarifa\taa hiyo ya check engine inaitwa oxygen sensor, IPO kwenye outlet manilfold na kazi take ni kuangalia hewa inayotoka ndani ya piston chember\sillinder kama imeiva\kuungua kwa 100%,

Kwa kawaida gari huvuta hewa safi na kuichanganya na petrol na kuichoma kwa spark plug ( kwa gari ya petrol) baada ya hapo huo moshi ndo unapita kwenye sensor inaangalia kama kuna kiasi cha oxygen bado hakijaungua ndo inatoa taarifa\taa hiyo.

Vitu vinavyoweza kusababisha gari kutokuchoma vizuri na kusababisha hiyo taa kuwaka
1: spark plug zinachoma chini ya kiwango
2: Mafuta yakuchakachua \vidumu.
3: uchafu kwenye mfumo wa mafuta\petrol filter. Na nozzle.
4: mfumo wa hewa \aircleaner ni chafu au mfumo wake hauko sawa: kwa kesi hii itaongezeka na taa nyingine zitawaka taa mbili:

Na wakati mwingine hakuna chochote! Ni sensor yenyewe tu imekufa inatakiwa uibadilishe,
Wakati mwingine haijafa ila imezidiwa na uchafu unaitoa na kuisafisha kwa petrol inakuwa mpya tena!

Haya mambo yanataka weledi ktk utatuzi wake, Shida inakujaga mwenye gari anataka asimamie na aone unatengeneza"

Diagnosis ni kifaa kinachoangalia hitilafu zinazohusiana na mfumo wa umeme ktk vifaa vilivyounganishwa kwenye huo mfumo tu.
Na sio kila kifaa cha umeme diagnosis itakisoma!

Ktk sababu nilizoziweka hapo juu zinazosababisha hiyo taa iwake diagnosis haiwezi kugundua hata moja!

Inaweza kutambua tu kama itakuwa sensor yenyewe ndo imekufa.

Kutibu tatizo vizuri panahitajika watu wawili, moja awe na weledi kwenye mfumo wa ingine na mwingine awe na weledi kwenye mfumo wa umeme na vipimo vyake.

Nk. Nk. Nk.........
 
Mkuu,taa ya check engine haiko hivyo. Huwa ni nyekundu,na ikiwaka huna ujanja. Zima gari tu livutewe. Vinginevyo engine inakufa instantly. Hiyo hapo mara nyingi ni taa ya sensor za umeme kama zina hitilafu. Mara nyingi hizo zinaweza kukupa muda mrefu kutumia bila ya wewe kuona chochote kilichobadilika ingawa gari inaweza kula mafuta,kukosa nguvu/pulling nk. Lakini ingekua ni TAA YA CHECK ENGINE,muda huu tungekua tunazungumzia Engine yako kunock!
 
Duh!,mi nilikua nadhani eti hii taa ndio ya Check engine...
 
Salam wadau. Taa ya check injini ya Toyota Coaster, model HDB50, engine 1HFE inawaka na kupoteza nguvu (accelerator haivuti) baada ya kutembea km kadhaa. Hali hii ina wiki sasa. Nimeipeleka gereji ili ikapimwe kwa kutumia mashine (OBD) na majibu yake ni kama yanavyoonekana. Pamoja na majibu hayo, wanashindwa kutatua tatizo. Naomba ufumbuzi katika hili
 

Attachments

  • IMG_20190430_141751.jpg
    154.4 KB · Views: 38
Kumbe hii sio Taa ya Check Engine?
Mbona Boeing 747 amesema ndio yenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…