point of correction..
Hiyo taa unayosema ipo kama birika na inawaka nyekundu si check engine...hiyo ni taa ya oil pressure na haiwaki kwa sababu oil imezidi au imepungua..
yaa hiyo ya oil presure inawaka endapo pump ya oil haiwezi kusukuma oil ipande juu kwenye sehemu za engine....na taa hii ya oil ikiwaka ni hatari sana zima gari na ulivute mpaka garage.
Hiyo taa ya orange inayoonekana kwenye picha ndiyo chek engine ikiashiria kuna kitu kwenye engine kina hitilafu....hivyo kwa ushauri mwenue gari akafanye diagnosis ili kubaini tatizo.
Point of correction! Uko sahihi, ukiona gari inawaka taa ya check engine tambua kuanzia hapo vitu vitatu vinatokea.
1: imeongeza ulaji Mafuta
2: imeongeza moshi (huuoni)
3: inamiss (huihisi)
Na wakati mwingine hakuna chochote kati ya hivyo na wala hakuna tatizo lolote kwenye mfumo isipokuwa tu ni sensor yenyewe ndo imekufa.
Sensor inayohusika kuleta taarifa\taa hiyo ya check engine inaitwa oxygen sensor, IPO kwenye outlet manilfold na kazi take ni kuangalia hewa inayotoka ndani ya piston chember\sillinder kama imeiva\kuungua kwa 100%,
Kwa kawaida gari huvuta hewa safi na kuichanganya na petrol na kuichoma kwa spark plug ( kwa gari ya petrol) baada ya hapo huo moshi ndo unapita kwenye sensor inaangalia kama kuna kiasi cha oxygen bado hakijaungua ndo inatoa taarifa\taa hiyo.
Vitu vinavyoweza kusababisha gari kutokuchoma vizuri na kusababisha hiyo taa kuwaka
1: spark plug zinachoma chini ya kiwango
2: Mafuta yakuchakachua \vidumu.
3: uchafu kwenye mfumo wa mafuta\petrol filter. Na nozzle.
4: mfumo wa hewa \aircleaner ni chafu au mfumo wake hauko sawa: kwa kesi hii itaongezeka na taa nyingine zitawaka taa mbili:
Na wakati mwingine hakuna chochote! Ni sensor yenyewe tu imekufa inatakiwa uibadilishe,
Wakati mwingine haijafa ila imezidiwa na uchafu unaitoa na kuisafisha kwa petrol inakuwa mpya tena!
Haya mambo yanataka weledi ktk utatuzi wake, Shida inakujaga mwenye gari anataka asimamie na aone unatengeneza"
Diagnosis ni kifaa kinachoangalia hitilafu zinazohusiana na mfumo wa umeme ktk vifaa vilivyounganishwa kwenye huo mfumo tu.
Na sio kila kifaa cha umeme diagnosis itakisoma!
Ktk sababu nilizoziweka hapo juu zinazosababisha hiyo taa iwake diagnosis haiwezi kugundua hata moja!
Inaweza kutambua tu kama itakuwa sensor yenyewe ndo imekufa.
Kutibu tatizo vizuri panahitajika watu wawili, moja awe na weledi kwenye mfumo wa ingine na mwingine awe na weledi kwenye mfumo wa umeme na vipimo vyake.
Nk. Nk. Nk.........