Msaada: taa ya Check engine inawaka

Msaada: taa ya Check engine inawaka

Paul Mchumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
1,039
Reaction score
1,256
Habari ya mida hii wana Jf
Nina gari yangu Passo,jana baada ya mvua mvua hizi zinazonyesha hapa mjini Dar,mara taa ya check engine imeanza kuwaka,sielewi tatizo ni nini,nikajua labda nikiizima then nikiwasha au ikikaa mpaka asubuhi ya leo taa itazima lakini wapi bado inaendelea kuwaka,lakini gari inatembea kama kawaida na hakuna utofauti wowote nilioubaini toka taa hiyo imeanza kuwaka,naombeni msaada wenu kama kuna mtu imeshawahi kumtokea hali kama hii au anajua chakufanya.
Natanguliza shukrani zangu!
IMG_20180409_071218.jpg
 
Inawezekana maji yamesababisha shoti ikakata fyuzi anza kwa kucheki fyuzi
 
pole sana ndugu yangu....kwanza hiyo taa kuwaka ni ishara kuwa kuna kitu kwenye mifumo ya injini hakipo sawa..ni sawa na mtu anapoumwa kichwa ni ishara ya dalili mbalimbali ambazo siyo nzuri katika mwili..inaweza mojawapo ya sensors za kwenye injini imezingua...inaeza ikawa sensor ya mfumo wa hewa au sensor nyinginezo..
nakushauri peleka gari gereji nzuri inayoweza kufanya diagnosis tatizo litabainika soon.
usiende kwa hawa mafundi gonga nyundo watazidi kuua injini na kukununulisha spea mpaka ujute.
Mimi nina nissan kwa mujibu wa user manual ya nissan yangu...check injini ikiwaka usiendeshe gari zaidi ya 80 kph....hivyo nakushauri endesha bellow 80kph.
usipuuzie hiyo taa mwisho wa siku utatumia gharama kubwa sana kutengeneza gari..yamewakuta wengi kwa kupuuzia hiyo taa kwa sababu waliona magari yao yanawaka kama kawaida.
Kuna baadhi ya mafundi wanaweza kukudanganya kuwa wanaweza ku- reset hiyo taa ila sikushauri...wanaweza waka reset ikazimika lakini kimsingi kama ni sensor imekufa tatizo litabaki pale pale na kuibua matatizo mengine..
Subiri wajuzi wengine waje wakuongezee maarifa.
 
kua makini kwenda gereji uchwara wakakata waya wa iyo taa ili izime na ionekane wame 'solve' tatizo , kuna bunch of sensors katika gari na moja ikizingua icho kitaa kinawaka,
 
Mara ya mwisho service ulifanya lini na wapi? Na ulifanya service gani? Tuanzie hapa.
 
Mara ya mwisho kubadilisha oil ni lini? Inawezekana oil imeshakaa muda mrefu hivyo imepoteza viscocity - η (ute ute)... Kama hujabadilisha muda mrefu, anza na kuchek oil...
 
Kuna mtu alinishauri nitoe temino za betry kwa dakika kama kumi hivi,then niwashe,nimefanya hivyo taa imezima mpaka leo haijawaka,nashukuru kwa ushauri wenu,ingawa imezima ila tapita nikafanye check up kwenye vipimo mlivyoshauri!
 
Kuna mtu alinishauri nitoe temino za betry kwa dakika kama kumi hivi,then niwashe,nimefanya hivyo taa imezima mpaka leo haijawaka,nashukuru kwa ushauri wenu,ingawa imezima ila tapita nikafanye check up kwenye vipimo mlivyoshauri!

ulichokifanya hapo ni kuifuta hiyo taa lkn ungepaswa kwanza kujua au fahAmu kwa nn au kipi kilisababisha taa kuwaka.??ndio uizime
 
PASSO ndg yang nakushauri tafuta mtu umuuzie hizo gari ni mbovu Sana kwanza zinatatizo katika mfumo wake wa sterling inaweza kugonga hadi ukachanganyikiwa
 
Acha LUNCH BOX (PASSO) welcome to BMW (full diet)
 
Mara ya mwisho kubadilisha oil ni lini? Inawezekana oil imeshakaa muda mrefu hivyo imepoteza viscocity - η (ute ute)... Kama hujabadilisha muda mrefu, anza na kuchek oil...

Tatizo limesababishwa na oil aliyoiweka. Huwa tunapeleka magari gereji yeyote tu ilimradi tumebadili oil. Kama viscosity ya oil uliyoweka sio yake hivi ni vitu hutokea, Nenda badili oil na utumie haswa oil za Total ndiyo kidogo afadhali na uweke kwa kiwango chake. Taa ikiendelea basi jua kuna hitilafu nyingine lakini mara nyingi husababishwa na oil uliyoitumia.
Oil nyingine huganda na kuzuia mipenyo ya oil.
 
Mimi Nina Rav4 Mayai inawaka hiyo taa mwaka wa 4 sasa lakini hakuna tatizo lolote
 
PASSO ndg yang nakushauri tafuta mtu umuuzie hizo gari ni mbovu Sana kwanza zinatatizo katika mfumo wake wa sterling inaweza kugonga hadi ukachanganyikiwa
Watanzania bhana[emoji16][emoji16][emoji16],mimi nimekaa na hiyo gari mwaka wapili sasa sijawahi pata hilo tatizo la sterling rack na ninakaa rough road...
 
Back
Top Bottom