Msaada: Taa ya tank la mafuta inawaka..

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
453
Reaction score
175
Habari wanajamvi,

Jana nilikuwa naendesha gari, bahati mbaya kulikuwa na foleni sana taa ya tank la mafuta ikaanza kuwaka,mafuta yalikuwa yameisha sana. Nilipofika kituo cha mafuta mafuta yalikuwa yameisha kabisa.

Nikajaza lakini taa ya kuashiria mafuta yanaisha bado inawaka bila kuzima. Je, hili ni tatizo na kama ni tatizo nini madhara yake?

Naomba msaada wenu wataalamu
 
kama kweli umeweka mengi ya kutosha kuzima taa... zima gari kabisa... SWITCH OFF afu ON washa gari na mshale utapanda na taa itazima
 
nimeweka mafuta ya 15,000/ na gari jana nilizima na leo asubuhi nimeiwasha naona bado inawaka.
 
nimeweka mafuta ya 15,000/ na gari jana nilizima na leo asubuhi nimeiwasha naona bado inawaka.

AAAh mkuuu ongezea mafuta 15000/= ni kama lita nane hivi, nadhani bado ina kiu iongezee tena mengine
 
umeweka mafuta kiasi gani...? coz kama yalikuwa yameisha kabisa inawezekana hayo uliyoweka ni kidogo so bado inakualert uongeze zaidi....

Kama nimemsoma vizuri anasema "kajaza", kwa mimi nachukulia ni full tank.
 
Mafuta ya 15,000/- kwa bei ya sasa 2,144/- ni lita 7 na taa huwa inawaka zikibaki litre 10 hivyo kama yakiisha kabisa kabisa inatakiwa uweke Litre zaidi ya 10 ili taa izimike...
 
nimeweka mafuta ya 15,000/ na gari jana nilizima na leo asubuhi nimeiwasha naona bado inawaka.

Sasa wewe umeweka mafuta lita 7 halafu kule juu umendika umejaza! unaleta utani? halafu unataka taa ya reserve izimike? tuondolee upuuzi hapa. Aliyekufundisha gari hakukufundisha vizuri!
 
AAAh mkuuu ongezea mafuta 15000/= ni kama lita nane hivi, nadhani bado ina kiu iongezee tena mengine
sawa mkuu lakini geji inasoma vizuri na mshale umepanda sehemu ambayo huwa haiwaki hiyo taa ya tank
 
nimeweka mafuta ya 15,000/ na gari jana nilizima na leo asubuhi nimeiwasha naona bado inawaka.

Ongeza mafuta ya kutosha acha ubahiri. Ukiruhusu hadi taa kuwaka kila wakati unaua pump.
 
Sasa wewe umeweka mafuta lita 7 halafu kule juu umendika umejaza! unaleta utani? halafu unataka taa ya reserve izimike? tuondolee upuuzi hapa. Aliyekufundisha gari hakukufundisha vizuri!

ndugu yangu Ribosome yamekuwa hayo,mbona waniambia maneno makali kiasi hiko.Samahani sana kwa kukosea nia yangu ilikuwa kutaka kufahamishwa.Samahani sana kaka mungu atatulipa kwa sote
 
Mkuu usipende kuendsha gari taa ikawaka kwa muda mrefu utasababisha matatzo mengine kwenye gari uenda ikawa lile boya lenye sensor limeshdwa kunyanyuka mafuta machache au kuna sensor imekufa.vilevile kuendsha aswa kwa haya magari ya kisasa yana kitu kinaitwa fuel pump ipo ndani ya tank so ukiendsha empty tank inaweza kuungua kwa sababu inavuta hewa.epusha kutu ktk tank kwa kuweka fuel daiy robo tank ni bora sana kuliko tank likiwa nusu ya robo
 
ndugu yangu Ribosome yamekuwa hayo,mbona waniambia maneno makali kiasi hiko.Samahani sana kwa kukosea nia yangu ilikuwa kutaka kufahamishwa.Samahani sana kaka mungu atatulipa kwa sote

Pole kama nimekukwaza, siku nyingine utajuwa kujielezea. ulisema umejaza, halafu baadae unasema nimeweka 15,000/=. Yote hiyo ni kutokupata mafunzo ya kutosha kuhusu uendeshaji wa gari, Watu kama wewe ndio huwa mnasabisha ajali za kijinga. Sasa gari ikikuzimikia sehemu ambayo ni hatari kuku overtake na magari yanabidi ya ku overtake, si inakuwa umewatakia watu ajali ya kipuuzi.
 
kwa kusoma comments za wengi nimegundua kwamba wengi wa waliotoa comments hawana experience na tatizo lililowasilishwa hapa jukwaani. Mimi nimeexperience hili, baada ya kujaza mafuta na kuona taa inaendelea kuwaka, ilibidi nichukue uamuzi wa kujaza full tank, na bado taa iliendelea kuwaka. Niliipeleka kwa mafundi, wakanambia itabidi kufungua tank na kuangalia sensor, lakini wakanambia haina madhara vile ilivyo, kikubwa nizingatie movement ya mshale wa mafuta tu. kwa zaidi ya miezi miwili hivi sasa natembelea gari yangu ikiwa na hii taa imewaka na sijaona tatizo. Nitakapopata hela nitaipeleka wakaangalie hiyo sensor kama imekufa au kuna tatizo lingine. Zaidi sana, nilishawahi kuwa na gari nyingine ambayo yenyewe taa ilizima tu ikawa haiwaki kabisa. Kwa hiyo ni juu yako kuangalia mshale unakwendaje. Lakini haikuwahi kuniletea shida yoyote, zaidi ya huo usumbufu wa namna ya kujua kiasi cha mafuta kilichomo kwenye gari. So kama haikupi shida nyingine yoyote, iache tu hadi hapo utakapopata nafasi ya kwenda kuitengeneza.
 
nashukuru kwa ushauri wako mzuri ntajitahidi kujieleza vizuri siku nyingine kaka.Zingatia kutokutumia hayo maneno yenye red yanachafua uzuri wa ulichoshauri.Natanguliza samahani kama na hapa nimekosea kujieleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…