nimeweka mafuta ya 15,000/ na gari jana nilizima na leo asubuhi nimeiwasha naona bado inawaka.
asante mkuu kwa maelezo mazuri na mifano halisikwa kusoma comments za wengi nimegundua kwamba wengi wa waliotoa comments hawana experience na tatizo lililowasilishwa hapa jukwaani. Mimi nimeexperience hili, baada ya kujaza mafuta na kuona taa inaendelea kuwaka, ilibidi nichukue uamuzi wa kujaza full tank, na bado taa iliendelea kuwaka. Niliipeleka kwa mafundi, wakanambia itabidi kufungua tank na kuangalia sensor, lakini wakanambia haina madhara vile ilivyo, kikubwa nizingatie movement ya mshale wa mafuta tu. kwa zaidi ya miezi miwili hivi sasa natembelea gari yangu ikiwa na hii taa imewaka na sijaona tatizo. Nitakapopata hela nitaipeleka wakaangalie hiyo sensor kama imekufa au kuna tatizo lingine. Zaidi sana, nilishawahi kuwa na gari nyingine ambayo yenyewe taa ilizima tu ikawa haiwaki kabisa. Kwa hiyo ni juu yako kuangalia mshale unakwendaje. Lakini haikuwahi kuniletea shida yoyote, zaidi ya huo usumbufu wa namna ya kujua kiasi cha mafuta kilichomo kwenye gari. So kama haikupi shida nyingine yoyote, iache tu hadi hapo utakapopata nafasi ya kwenda kuitengeneza.
ndugu yangu Ribosome yamekuwa hayo,mbona waniambia maneno makali kiasi hiko.Samahani sana kwa kukosea nia yangu ilikuwa kutaka kufahamishwa.Samahani sana kaka mungu atatulipa kwa sote
asante mkuu ntafanya hivyokilichotokea kwenye gari yako umetembea na mafuta ya reserve taa inavyoanza kuwaka huwa inakuwa njano pale unakuwa na mafuta kiasi cha 5ltr ikiwaka moja kwa moja inamaanisha unatumia hayo mafuta ya ziada.sasa basi ukiweka mafuta litre 5 taa inaendelea kuwaka unatakiwa uweke lt 7-10 kwa gari iliyoisha mafuta kabisa na baada ya kuweka mafuta unazima gari na kuwasha tena.fanya hivyo mkuu
kilichotokea kwenye gari yako umetembea na mafuta ya reserve taa inavyoanza kuwaka huwa inakuwa njano pale unakuwa na mafuta kiasi cha 5ltr ikiwaka moja kwa moja inamaanisha unatumia hayo mafuta ya ziada.sasa basi ukiweka mafuta litre 5 taa inaendelea kuwaka unatakiwa uweke lt 7-10 kwa gari iliyoisha mafuta kabisa na baada ya kuweka mafuta unazima gari na kuwasha tena.fanya hivyo mkuu
AAAh mkuuu ongezea mafuta 15000/= ni kama lita nane hivi, nadhani bado ina kiu iongezee tena mengine
Kama nimemsoma vizuri anasema "kajaza", kwa mimi nachukulia ni full tank.
Daah😁😁😁Unavyopita na kutumwagia maji machafu halafu upo tinted unakula a/c ulikua unaona raha? Jaza wese hilo 15 ni lita chache sana kwa gari ongeza ya 35 tena,kama umeanza mwendo huo lazima uipaki gari juu ya mawe!!!