kwa kusoma comments za wengi nimegundua kwamba wengi wa waliotoa comments hawana experience na tatizo lililowasilishwa hapa jukwaani. Mimi nimeexperience hili, baada ya kujaza mafuta na kuona taa inaendelea kuwaka, ilibidi nichukue uamuzi wa kujaza full tank, na bado taa iliendelea kuwaka. Niliipeleka kwa mafundi, wakanambia itabidi kufungua tank na kuangalia sensor, lakini wakanambia haina madhara vile ilivyo, kikubwa nizingatie movement ya mshale wa mafuta tu. kwa zaidi ya miezi miwili hivi sasa natembelea gari yangu ikiwa na hii taa imewaka na sijaona tatizo. Nitakapopata hela nitaipeleka wakaangalie hiyo sensor kama imekufa au kuna tatizo lingine. Zaidi sana, nilishawahi kuwa na gari nyingine ambayo yenyewe taa ilizima tu ikawa haiwaki kabisa. Kwa hiyo ni juu yako kuangalia mshale unakwendaje. Lakini haikuwahi kuniletea shida yoyote, zaidi ya huo usumbufu wa namna ya kujua kiasi cha mafuta kilichomo kwenye gari. So kama haikupi shida nyingine yoyote, iache tu hadi hapo utakapopata nafasi ya kwenda kuitengeneza.