Msaada - Taarifa za Muhimu juu ya Safari

Nauli ya basi Makambako mpaka Songea ni elf 20 (5hrs) songea to Tunduru hakuna basi kubwa bali kuna landrovers nauli elfu 22(rough road).
Mwisho kwa tahadhari zaidi zingatia ulinzi na umakini mara uwapo songea, ukiwa bar, hotel, njiani acha kujionyesha kama ni mgeni sana au una pesa nying kwani huu mji kwa mauaji ndo usiseme.
Umeona yanayojiri leo.
 

Nashukuru Mkuu Kayako; kwa hiyo njia ya Songea - Tunduru magari makubwa hayawezi kupita?, kwa nini hakuna mabasi makubwa yanayopita njia hiyo - abiria ni wachache au njia ni mbaya sana?.
 
Nashukuru Mkuu Kayako; kwa hiyo njia ya Songea - Tunduru magari makubwa hayawezi kupita?, kwa nini hakuna mabasi makubwa yanayopita njia hiyo - abiria ni wachache au njia ni mbaya sana?.
Njia ni mbaya sana...kipindi cha mvua ni worst!
 
Hivi White house siku hizi siyo famous tena...? halafu huko msamala ni nje sana ya mji!
 
Wakuu waliotangulia wameelezea vizuri sana Idodomya-Iringa-Makambako, just kuongezea tu: huwa kuna baridi sana hasa Mafinga (Mufindi) na Makambako...kipindi hiki yaweza kuwa nafuu kidogo

Makambako-Songea: angalieni sana milima ya Lukumbulu, kuna milima, ngema, mabonde na kona za kutisha...na hii ni kuanzia Madaba (km chache tu baada ya makambako) hadi unaingia Songea. Kama mna gari binafsi na dereva ni mgeni basi inabidi awe makini sana maeneo hayo, very lonely place....inatisha tisha kimtindo.

Songea-Tunduru barabara ni vumbi halaf very rough.

Sina uzoef na masasi lakini ukiwa unatokea kusini kuelekea Dar, maeneo mengi ni lami....kuna eneo moja katika wilaya ya Kilwa linaitwa Nyamwage halina lami barabara bado inajengwa, ni pabaya sana hasa wakati wa mvua...kama gari haina 4wheel lazima mbaki hapo.
Kibiti si mjini sana. Ni kakitongoji tu na hakuna guest house "za maana", hakuna inayozidi 10,000. Walau mngelala Ikwiriri ningekuelekeza guest ya ukweli kiasi kwa maeneo hayo. Kutoka Ikwiriri hadi Kibiti ni kama km20 hivi.

Bagamoyo: very common nadhani hata uki-google waweza kupata habari zake. Msisahau kupita pale Kaole mkapate historia ya mambo ya kale.
Kuelekea Same mtapita barabara kuu ya dar-chalinze-segera-korogwe-mombo (unless kama mtapitia bagamoyo msata road). Maeneo mazuri ya kupata chakula huwa aidha Korogwe au Mombo. Mabasi mengi husimama maeneo hayo. Lakini pale Korogwe kuna hotel nzuri sana pale dar express, wana chakula kizuri. Kama mnapenda nyama (mbuzi) choma mkale Mombo stendi. barabara ni lami lkn nyembamba, dereva awe makini kuna ajali nyingi za barabarani maeneo hayo.
Hedaru-Same pamenyooka lakini kuna upepo mkali sana...mtakutana na mabango ya warning.

What else....
Ohh Arusha...dah! watakuja watu wa Arusha kukueleza vizuri mana wapo wengi humu mi nikisema naweza kudanganya.
Tarangire sijajua kama mnakwenda mbugani au...
Mbuga hii ndo inaongoza kwa kuwa na tembo wengi.
Tarangire ni mahali pakame sana, hata hayo maeneo ya babati ni makame sana.

Dah! i hav to go, nitarud later.
 
Usisahau kubeba camera ututumie masinepu ukirudi.........tuijuwe nchi yetu vizuri
 
Njia ni mbaya sana...kipindi cha mvua ni worst!

Asante Mkuu Mkeshaji; nafikiri kipindi cha mvua huko ni Nov - May. Vipi katika miezi mingine unaweza kupita na gari kubwa kwa shida au haipitiki kabisa. Kama haipitiki kabisa vipi mazao wanasafirisha vipi au huko hakuna bidhaa yeyote inayozalishwa?? Sitaki kujipatia majibu mepesi kwa swali gumu kama hili, samahani mkuu...!!!
 
Kwa magari ya abiria wengi wanaogopa kupeleka mabasi yao huko kwa sababu ya barabara. Walau Landrover "zina roho ngumu" ndo mana zinaweza kwenda huko.
Magari ya mizigo yanakwenda kwa sababu si lazima yafike kwa siku moja.
 
Nakushukuru Mkeshaji; kwa taarifa za ziada kutokea Dodoma mpaka Songea. Hizi taarifa zinanisaidia kupanga safari yangu vizuri zaidi; asante kwa kunieleza kwamba kibiti ni mji mdogo na ninaweza kukosa guest house. Nakubalina na wewe na sasa nitapanga kulala Ikwiriri, haya maeneo nilishawahi kupita lakini zamani kidogo. Nakumbuka tulikuwa tunatokea Mtwara na landrover 109, ilitusumbua sana tokea Lindi mpaka Nangurukuru, huwezi amini hapo tulitembea usiku kucha na Nangurukuru mpaka kivukoni (kabla ya daraja) tulitumia mchana wote; hivyo basi tuliamua kulala ikwiriri, lakini kulikuwa giza hivyo sikupata hata kujua uzuri na ubaya wa mji huo, kwani tuliondoka alfajiri sana.

Kutoka Bagamoyo tutapita ile njia inayotokea Msata. Tarangire tunataka kwenda mbuga za wanyama, sijajua connection ya Tarangire - Ngorongoro iko vipi, naamini wakiingia watu wa Arusha wanaweza kunipa taarifa nzuri zaidi, ili ikiwezekena nipitie na Ngorongoro.
 
Usisahau kubeba camera ututumie masinepu ukirudi.........tuijuwe nchi yetu vizuri

Haswaaa...!!! kusudi ni kuijua nchi yetu, nitajitahidi kupata picha za kutosha, vile vile naangalia uwezekano wa kutengeneza japo ka-documentary kadogo juu ya safari hii; siyo wazungu ndiyo wanakuja hapa na kututengenezea documentary za kutuonyesha uzuri wa nchi yetu.
 
Kibiti zipo guest house lakini si nzuri sana.
Ukifika Ikwiriri ulizia Migude guest house, ni guest nzuri na salama kuliko zote hapo Ikwiriri, chumba ni self kwa sh. 10,000/- ila hawaruhusu kulala na mwanamke ambaye si mkeo (lazima uoneshe cheti cha ndoa)...ni ya masista hii.

Kwa upande wa barabara sasa hv maeneo mengi ni lami kasoro vipande vichache tu. Nangurukuru hadi Somanga ni mkeka then unaanza vumbi hapo Somanga, Mohoro hadi Nyamwage (mwendo wa saa 1.5 ) then unaanza lami just before Ikwiriri hadi dar hiyo.
Ikwiriri sasa hv kuna umeme unaotoka Somanga pale kwenye mtambo wa gesi.

Unaweza ukatoka Arusha asubuhi then ukatembelea Tarangire then mkageuza kwenda lake Manyara halafu ukalala mto wa Mbu. Asubuhi inayofuata ukaenda Ngorongoro crater kama utapenda. Kwenda Ngorongoro lazima upite lake manyara..nilishawahi kufanya hivyo miaka mingi sana iliypita.

Kuhusu kulala Arusha unaweza ukapata lodging kuanzia 20,000/- na kuendelea, iantegemea na mfuko wako/hadhi yako na preference. lakini kuhusu suala la kulala Arusha nadhani ungewasiliana na watu wa Arusha wanaweza kukushauri vizuri.
 
Nimewahi kufika Arusha na kupata mahali pa bei rahisi zaidi pale hostel za Centre for Educational Development in Health, Arusha (CEDHA) kiko chini ya wizara ya Afya mbele tu ya Naura Springs Hotel ukiwa kwenye main road ya kwenda Namanga. Hii ilikuwa mwaka 2008 na bei ilikuwa 12,000/= kwa chumba kizuri. Kama wewe ni mfanyakazi wa umma ni rahisi zaidi kupata. Waweza kumpigia simu dada mmoja anaitwa Oliva nitaku-PM namba yake au bosi wake ili kufanya booking mapema. Ni mahali salama kabisa na parking ya kutosha ila ikivuka saa 2:00 usiku hupati chakula pale inabidi utoke nje si mbali ni ng'ambo tu ya barabara kuu ya DAR-Namanga kuna restaurants nyingi na nzuri kabisa.
 
Kama wengine waliotavyotangulia kusema, barabara ya Dodoma - Iringa via Mtera ni ya vumbi na kuna milima maarufu ya Nyang'oro baada ya kutoka Mtera. Usishangae kuona kama unarudi ulikotoka wakati unaelekea Iringa kutokana na barabara ilivyo sababu ya ile milima. Unahitaji kuwa na dereva mzoefu wa safari ndefu na maeneo ya kutisha kidogo kama hayo maana anaweza kupaki gari pembeni na kukwambia "siwezi kuendesha nahisi kizunguzungu". Sehemu ile pia ina mawe makali yanayopasua tairi kwa sana kwahiyo hakikisha kuwa gari lako halina tairi za mchina. Na uwe na spea za kutosha vingivenyo mtalala hapo milimani.

Kwa Iringa - Songea kulala Makambako ni karibu sana mnaweza kusogea hadi Njombe (45 kms more) ambao mji mkubwa kidogo na mnapata mahali pazuri pa kulala pale.
 
Wanajamii wa Arusha vipi au ndio hamtaki tuwatembelee...!!!!???, taarifa zaidi juu ya mbuga za wanyama (Arusha National park, Tarangire, Lake Manyara na Ngorongoro)
 
Hakuna wanajamii wanaishi mikoa ya Mtwara na Lindi kutupatia taarifa za vivutio katika mikoa hiyo, vipi lile eneo lililopatwa na mafuriko makubwa miaka ya 90, kuna historia yeyote inaweza kupatikana?. Kuna eneo nje kidogo ya mji wa Lindi kuelekea Mnazi Mmoja kulikuwa na mashamba ya chumvi, vipi bado yapo?. Nje tu kidogo ya mji wa Lindi kuelekea Nangulukulu kulikuwa na kilima kikali (Nafikiri panaitwa - Mng'ong'o) ambapo magari yalikuwa yanaanguka sana, vipi hilo eneo lilifanyiwa marekebisho maana ilikuwa katikati ya kilima kuna kona kali. Vipi samaki wa Nangulukulu...???
 
Wanajamii wa pande za Arusha mpooooooooooo......!!!!!
 
Wanajamii wa pande za Arusha mpooooooooooo......!!!!!
 
Tunajifunza mengi humu JF. Hii itatusaidia na sisi wengine tutakapopita maeneo hayo.
 
Tunajifunza mengi humu JF. Hii itatusaidia na sisi wengine tutakapopita maeneo hayo.

Mgombezi,

Kama utajaliwa kusafiri na kufika Songea, nifanyie yafuatayo njiani unapokwenda Tunduru;Uliza mito yote ya maji isiyokauka na ukipata majina yake itakuwa poa. Kisha nitumie.
 
Mgombezi,

Kama utajaliwa kusafiri na kufika Songea, nifanyie yafuatayo njiani unapokwenda Tunduru;Uliza mito yote ya maji isiyokauka na ukipata majina yake itakuwa poa. Kisha nitumie.

Asante Malila; kwa kunikumbusha vitu vya msingi vya kuangalia. Kwa kweli nina mpango wa kutengeneza documentary ambayo itaweza kuwa na taarifa mbalimbali, naamini zitakuwa msaada. Ukikumbuka dondoo yeyote ile kaka nimwagie hapa, nitaendelea kutoa update mpaka maandalizi yatakapokamilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…