Msaada tafadhali,binti kagundua mme mtarajiwa anaigiza ulokole, kumbe .......!

Hapo tunatafuta njia ya kuairisha ndoa,ikishindikana hakuna jinsi ni bora aibu kuliko ndoa.
 
Mwenye pesa shetani makanisani kwa walokole anatengewa siti ya mbele kabisa ili iwe rahisi kutoa maburungutu ya sadaka.
Shetani wa pesa ana nguvu, si umeona wakwe wameng'ang'ania binti yao aolewe ili misaada ya shetani iendelee kumiminika
Sawa nakubali shetani yupo ila hawezi kushinda nguvu ya mungu hasa hasa anaijaribu tu,ndio maana mungu kamfunulia jen ubaya wa huyu mtu mapema kabla ya ndoa!
Na siku mungu akiamua kumuumbua shetani ndio km hv jamaa ukweli ukiwa wazi kazi yake kwisha!
 
Aisee mpe Jen pole sana.

Nikirudi baadaye ntamshauri cha kufanya.

Hamjamboni mabibi na mabwana?

Cantalasia mambo?
Shikamoo babu ODM!
Pole imefika,ila nakusubiri babu utoe andiko lako hapa lol!
 
Unafikiri huyo tajiri angemwambia jeni kuwa hajaokoka angempata jeni? na hakika asingempata na mabinti wa siku hizi ukimwambia ukweli tu anakukimbia mabinti wa siku hizi wanapenda kudanganywa jamaa nae amenitumia style hiyo
 
Mtandao wa Jinsia, TGNP, TAWLA nk wanasoma humu au wajulishwe mapema waingie kazini, namwonea huruma binti/dada yetu!
Nimekusoma na umenikumbusha kitu,ngoja kuna mtu niongee naye anahusika kbs!asante mkuu!
 
Unafikiri huyo tajiri angemwambia jeni kuwa hajaokoka angempata jeni? na hakika asingempata na mabinti wa siku hizi ukimwambia ukweli tu anakukimbia mabinti wa siku hizi wanapenda kudanganywa jamaa nae amenitumia style hiyo
Ndio ajiaandae kuumbuka,na ndio atajua mungu ni zaidi ya shetan na pesa zake!
 
Hahahaha muhailishe ndoa?????????????? jeni ni kigeu geu na posa wakwe wamesha kula
Walikuwa hawajui bwana,unafikiri jamaa angekuwa mkweli jen angekubali?wala asingekubali na wasingefikia huku kote!
 
HAYO NDO MADHARA YA WAZAZI WETU KUZAA WATOTO ILI WAJE WAWALETEE RETURNS(MAHELA) TOFAUTI NA WENZETU WA MBELE WANAZAA MTOTO kutokana mshiko wa kumlea na ku mprovidia mahitaji yake muhimu hatimaye wanamuacha ajiamulie akiwa huru kujiamulia mambo yake mwenyewe akiwa mkubwa.
 
Walikuwa hawajui bwana,unafikiri jamaa angekuwa mkweli jen angekubali?wala asingekubali na wasingefikia huku kote!

jeni si alikuwa anataka ndoa? na msimamo wa wadada wengi hata kama anatongozwa na chizi au mvuta bangi huwa inakuwa wanataka aende kwa wazazi kisha ndoa sasa jeni ni kigeu geu jamaa ametimiza yote leo anasema hamtaki kwa vile jamaa sio mlokole
 
Uko sahihi kbs mkuu!
Hela shetani.
 
Unafikiri huyo tajiri angemwambia jeni kuwa hajaokoka angempata jeni? na hakika asingempata na mabinti wa siku hizi ukimwambia ukweli tu anakukimbia mabinti wa siku hizi wanapenda kudanganywa jamaa nae amenitumia style hiyo
Wala jeni sio kigeu geu,tatizo ni uongo wa jamaa,kwann asingekuwa mkweli ili km jeni anamkubali, basi amkubali akiwa anajua ni mtu ambaye hajaokoka na nayeuza hayo mavitu kwan kungekuwa na shida gani?uongo ndio tatizo!
 
jen akaendelea kuwasiliana na jamaa na wakawa marafiki akamkaribisha kanisani kwao jamaa akawa anakuja mpaka naye akaokoka

Jeni aliamua kumbadilisha msimamo wa kidini jamaa mpaka akakubali na akaokoka na kubatizwa kwa maji mengi leo jeni anamgeuka na kumwona jamaa hafai sio mlokole kamili hivi kuna kipimo cha ulokole? jeni alimpa jamaa test afanye akachemka leo jeni anaconclude jamaa hafai kumwoa jeni? basi nyie marafiki zake mmemwonea wivu jeni na kumshauri vibaya apige teke bakuri la dhahabu
 
Fidel80!!!!!!,ww haya,huyo jamaa ameongea mwenyewe kwenye simu kuwa karibia anamaliza kifungo cha ulokole feki,so alijikubalisha kuokoka kinafiki na kudanganya watu ndio maana jen amekasirika!
Mbona hakulazimishwa alijidai neno limemuingia na kukubali kmpokea yesu kumbe alikuwa anaigiza!
Hakuna wa kumtaka huyo mzungu wa unga tapeli,wala hana udhahabu wowote!
 
Inasikitisha .. Mwambie dada jenny ajaribu kuwa convince wazazi kwamba jamaa hafai.... pia mambo ya kulazimishana ndoa yameshapitwa na wakati..
 
ndoa hailazimishwi hata siku moja. hakuna kufunga wala kuomba, kwani Mungu ameshaweka wazi kila kitu. Jeny aache kuwasiliana na huyu jamaa amkane kwa uwazi. hao wanaoendelea kumwombea jeni waendelee na maombi yao. siku ifkifika hawatamlazimisha kufanya agano la ndoa na huyo mjamaa.

onyo kwa Dada zetu:
msikubali lift ovyo na hata kuzoewa ovyo. mvua haiui, siku ile angenyeshewa tu hakuna tatizo kuliko hii njia panda aliyoingia sasa. wewe mtu humjui anakwambia upande gari yake wewe unapanda, hivi inawezekanaje?. Ashukuru amemvutia pumzi maana siku ileile angesha.... hata hii ya kubadilsihana contact na mtu humjui, ya nini? ivi duniani hapa watu unaowafahamu ni wachache sana kiasi cha kutaka contact mpya zisizo hata fahamika zitokako???. tujifunze kuwa sisi wenyewe. mara nyingi dada zetu huwapuuza watu ambao mnawafahamu, halafu mnaanguka kwa mijitu hata haifahamiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…