Msaada tafadhali,binti kagundua mme mtarajiwa anaigiza ulokole, kumbe .......!

hujasema kama njemba ilifanikisha azma yake au lah, poor jane, hapo sijui kama atataka tena kusikia mchumba maana atajua ni wale waleeeeeeee! mijanaume mingine bwana, ni kazi kutuharibia sisi tulio waaminifu, hovyo sana
 
Inasikitisha .. Mwambie dada jenny ajaribu kuwa convince wazazi kwamba jamaa hafai.... pia mambo ya kulazimishana ndoa yameshapitwa na wakati..

Ni kweli kbs,but ndio tunatafuta namna ya kuwashawishi hao wazazi waelewe japo wakubali hata ndoa iairishwe huyu jamaa aulizwe!
 

Kinachotakiwa hapo ni watu kama ww ambao tayari wanajua kinachoendelea kutoa taarifa kwenye uongozi wa mtaa kwani hiyo ni kama kulazimisha ndoa isiyo ya ridhaa ya upande mmoja yaan wa JENI, yaan CANTALISIA ww kama kweli umeingiwa na huruma juu ya kinachoendelea fanya ivyo ukishirikiana na wale mawifi wa JENI kwani hata kaka yao atawaelewa tu,mbona mtakuwa Heroes Kwa JENI na kwangu pia
 
Toeni ripoti kwa mamlaka husika kuhusu jamaa kama kweli ni muuza unga na atafatiliwa tu. Pili huyo binti amkatae altareni kama hakuna njia mbadala maana akisema I DONT badala ya I DO inaweza kusaidia mambo yasiendelee mbele.
 
Huyo binti anatakiwa atoroshwe-then aje aonekane baada ya tarehe ya harusi kupita-hao wazazi wake akiwaendekeza atakuja kujuta maisha yake yote,
MSAIDIE KWA KUMTOROSHA
 
Najua kinachpaswa kufanyika hapo ni mgogoro huu kuingiliwa na mtu wa tatu (3rd party) nje ya familia.Jeni aseme anahitaji kuongea na mchungaji angalau na wazee wa kanisa wenye kuheshimika sana ktk kanisa hilo.Atoe ukweli wake.Tena kama mwana JF mmoja alivyosema kwamba ni risk kwa kuyasema hayo, ila mungu aliyemfunulia maono hatomwacha kabisa atamwonesha njia.Mie ndhani kwa vile wazazi ni walokole na kwa vile wanamwombea akimtaka mchungaji wazazi watamsikiliza.
 

binafsi naona ushauri wangu ni mzuri kabisa..
Hatoki ndai kafugiwa , hawezi kuongea na wazazi wake
wakamwelewa, ni analazimishwa kuolewa na mtu ambaye
hampendi khaaaaa. kilichobakia ni yeye kuwa mkweli na nafsi yake..

binafsi nadhani afanye awezalo kutoka kwenye hili balaa..
na muda mbae kila mtu atakuwa anamsikiliza ni pale akiwa
kanisani wakati wa "I DO" aseme tu ukweli au asema hataki
kuolewa....
 
Aendelee na mipango ya harusi lakini siku ya harusi amkane mbele ya madhabahu!
 
Mimi ninafikiri hao wazazi wanahitaji maombi. Wao ndio walioingiliwa na mapepo.
 
Inasikitisha .. Mwambie dada jenny ajaribu kuwa convince wazazi kwamba jamaa hafai.... pia mambo ya kulazimishana ndoa yameshapitwa na wakati..
Hicho ndio tunachoomba kwan wazazi mpaka jana jion bado wamekomaa wanadai kuwa watu wanawaonea wivu ndio maana wanamjaza mtoto wao maneno ya uongo ili asiolewe!
 
Uko sahihi kbs kindimbajuu,yani km siku ile angempotezea wala haya yote yasingemfika!
kwa upande wa wazazi mpaka sasa hawaelewi kitu na jeny jana usiku ameshamwambia huyo mchumba waairishe ndoa mpaka mwakani kwan kuna mambo anataka ayafahamu kuhusu huyo bwana,jamaa hakuibu na akakata simu na haikupatikana mpaka asubuhi ya leo!
 
hujasema kama njemba ilifanikisha azma yake au lah, poor jane, hapo sijui kama atataka tena kusikia mchumba maana atajua ni wale waleeeeeeee! mijanaume mingine bwana, ni kazi kutuharibia sisi tulio waaminifu, hovyo sana
Siku ile hakufanikisha,ndio hivyo km hili litapita itamchukua mda sn kusahu,pole zenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…