Msaada tafadhali,binti kagundua mme mtarajiwa anaigiza ulokole, kumbe .......!

Ni kweli kbs,kuna watu fulan wa mambo ya kisheia tumeongea nao na leo wataenda kuongea na jeny pamoja na wazazi wake then kuanzia hapo ndio mambo mengine kuhusu hiyo ndoa yatafuata ila wamehakikisha jeny hawezi kuolewa kwa lzm.
 
Toeni ripoti kwa mamlaka husika kuhusu jamaa kama kweli ni muuza unga na atafatiliwa tu. Pili huyo binti amkatae altareni kama hakuna njia mbadala maana akisema I DONT badala ya I DO inaweza kusaidia mambo yasiendelee mbele.
Uko sahihi kbs mkuu,hilo tumeshalifanya na watu hao wanaenda kuonana na familia ya jeny leo.
 
Huyo binti anatakiwa atoroshwe-then aje aonekane baada ya tarehe ya harusi kupita-hao wazazi wake akiwaendekeza atakuja kujuta maisha yake yote,
MSAIDIE KWA KUMTOROSHA
Tumeshaongea na watu wakisheria na wamekubali kulishuhulikia swala hili na wataonana na familia ya jeny leo!
 
Uko sahihi hilo limeshaanza kushuhulikiwa,japo jana usiku jeny aliongea na jamaa na akamwabia anataka arusi iairishwe mpaka mwakan kwan kuna mambo anataka ayafahamu vizuri kuhusu jamaa,hapo jamaa akakata cm na hajapatikana mpaka asubuhi hii!
 
Ni sawa kbs my dia,hope ufumbuzi utapatikana kabla hata ya siku ya ndoa,coz kuna watu tumeongea nao wameahidi kulishuhulikia kuanzia leo.
 
Jen hana namba za wachungaji wake? Kawaida namba za wachungaji siyo siri makanisa mengine wanazitangaza kila jpili.. Pamoja na kuwa wamepatikana watu wa kisheria, wekeni hapa namba za wachungaji wake tuwasiliane nao, wakipata maelezo kama uliyoweka hapa hakutakuwa na ndoa hapo.
 
Kuweni wakweli jamani, hivi kuna mwanamke anakataa kuolewa!?
Baba huo ndio ukweli,si kolewa kuongeza idadi ya walioko kwenye ndoa bali ni kuolewa na mtu unaempenda na kuifurahia ndoa yenyewe!
Km ni kuolewa tu kuongeza idadi ya waliolewa hata mie ungekuta siku nyingi sn nishakuwa kwenye idadi!
 
jeni anatakiwa aangalie uhalisia wa jamaa na akae nae ... pia ashukuru kamwelewa kabla hawajaingia kwenye ndoa isipokuwa jeni na wazazi wake walikuwa na haraka sana kwa suala la ndoa na pia umri wake ungali bado
  1. anatakiwa atafute wazee wa kuweza kuwakilisha mawazo yake kwa wazazi wake
  2. aongee na mchungaji suala zima aliloliona na aweze kuthibitisha
 
Nikweli hili swala lilimefanyika kwa urahisi sn,tatizo sijui ni hela na misaada huyu jamaa alizokuwa nanatoa,kwa akina jeny na kanisan,maana gafla kanisani wakamuamin na wazazi wakamuamin.
Kuna watu wamekubali kulishulikia na leo wataongea na wazazi wa jeny.
 
Jamani ndugu zangu hilo suala mbona rahisi sana
1. Jamaa aitwe nyumbani Jen aseme ya moyoni mwake na kijana yule aaibishwe mbele ya wazazi ikiwa ni pamoja na kumvua shati hayo matattoo yaonekane, we utaolewajwe na mtu anamatattoo? hiyo ni miungu yake na Jen ana Mungu mwingine kwa kweli haitowezekana. Lakini hilo tendo linaweza kuwa hatarishi kwa Jen na familia yake kwani jamaa anaweza akarevenge, sasa wakifanikiwa kwa hilo, waende polisi wakaombe protection order au kukata RB kabisaa

2. Ikishindikana kumwita jamaa nyumbani, nyie rafiki zake ambao mmeushuhudia huo uhalisia wa huyo jamaaa basi nendeni polisi mkafile a security order hiyo itashinikiza Jen kuachwa huru na wazazi na huyo jamaa kutomsogelea tena zaidi muwambie na polisi juu ya hizo tetesi za madawa ili wamfanyie uchunguzi wa kina, hapo atakaa mbali nae na wazee watapata fundisho, alaa!!
Huu utaratibu wa kuchaguliana wenza umerudi lini tena, alaa!
 

tatizo wengi wanaamini mapenzi lazima kiwepo kitu cha tatu ambacho ndicho kitakuwa msingi mfano uwezo wa kipesa, imani, etc lakini unaweza kukutahakuna mapenzi na jeni na wazazi wake nadhani wamefuata zaidi imani na pesa za jamaa lakini hawakufikiria utu wa mtu na hayo ndio matunda
 
UKO sahihi mkuu,tayari tumeshaanza kulifanyia kazi hope mungu atasaidia.
 
Unajua BPM humu aishan kila mtu ana kitu anakihitaji au kukipenda hasa ktk mambo ya relation,ukiachia swala la hela iman nayo ni kitu kigumu kukibadilisha kwa mtu.
Naamin hivyo kwa upande wa jenny naoina yeye yuko kiiman zaidi na wazazi wananichanganya nahisi wako pande zote za iman na kipato.
 

mkuu ulichosema ni sahihi lakini suala bado liko kwa jeni maana inaonekana yuko kisiwani hana mtu anayeweza kumsimamia kuanzia kwa wazazi na kwa wachungaji ambapo itajengwa hoja ya jeni kuaminika na nini ambacho kinatakiwa kiwe

ila suala la polisi kwenda kushtaki inaweza ikajenga chuki zaidi ila kama walikula cha jamaa lazima wawe na hofu
 

lakini katika imani hiyo imekuzwa na misaada ya kibinadamu ambayo imeangaliwa kama imani
 
Hapo ndio palikuwa pa muhimu na kwa hakika ametimiza wajibu wake...hili la kuongea na wazazi sasa litakuwa rahisi tu.
 
Uko sahihi hilo limeshaanza kushuhulikiwa,japo jana usiku jeny aliongea na jamaa na akamwabia anataka arusi iairishwe mpaka mwakan kwan kuna mambo anataka ayafahamu vizuri kuhusu jamaa,hapo jamaa akakata cm na hajapatikana mpaka asubuhi hii!

cantalisia je ni hoja gani aliyojenga kwa jamaa?? maana ikiwa na uwalakini kitamshtua huyu bwana , na kama hoja ya jeni ni kumfahamu jamaa zaidi hapo atakuwa amekosea kwani ategemee presha kubwa sana kutoka kwa jamaa akiwa na dhamira ya kutimiza lengo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…