Msaada tafadhali: Gharama za ujenzi wa banda hili

EWGM's

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
1,521
Reaction score
2,112
Waungwana kwa wale wenye uzoefu naomba muongozo tafadhali. Nataka kujenga banda kama hilo hapo chini lenye ukubwa wa (5X20). Nina kashamba kangu kapo Msata njia ya Bagamoyo nilitaka nimwekee mama yangu mradi aanze ufugaji wa bata mzinga. Hivyo nilitaka kujua makadirio ya gharama za ujenzi na vifaa zenye kukaribiana na uhalisia.Nataka nimjengee mapema iwezekavyo kuanzia sasa, tafadhali mchango wako wa mawazo unakaribishwa. Ahsanteni

farm-chicken-412.jpg

N.B. Samahani kwa usumbufu wowote utakao tokea ahsanteni
 
Wanandugu naombeni mawazo yenu jamani,

Mkuu hiyo nyuma sio ndogo, ni kubwa sana, Kwa kukusaidia na makisio ya Kawaida tu ni Kama ifuatavyo:Hapa ni kwa mbao za treatedMbao za boma= 1080000/Mbao za kenchi 2x2 na 4x2=1584000Bati=1280000Floor (kokoto, mchanga, cement) =1300000Jumla ndogo= 5244000 ( bila kuweka gharama za wavu, mafundi, usafiri, misumari, ulinzi na gharama zingine zilizojificha) 1: Gharama inaweza kupungua kama ukinunua vitu reject pale Tazara- Buguruni, kuna kila kitu pale2:ukitumia mbao zisizokuwa treated unabidi upake dawa ya mchwa( dudu killer), na tatizo kubwa la hizo mbao huwa ni fupi, hivyo itakubidi ununue mbao mbili kwa kipande ambacho kingeweza kuzibwa na mbao moja ya treatedNimekosa muda, ningekuwekea na idadi ya material yanayotakiwa, lakini hilo banda sio chini ya 5.5 mil
 
Sorry, niliweka space na paragraph lakini sjuhi imekuwaje
 
[QUOThapa GM's;775371QUOTEZE=3]Waungwana kwa wale wenye uzoefu naomba muongozo tafadhali. Nataka kujenga banda kama hilo hapo chini lenye ukubwa wa (5X20). Nina kashamba kangu kapo Msata njia ya Bagamoyo nilitaka nimwekee mama yangu mradi aanze ufugaji wa bata mzinga. Hivyo nilitaka kujua makadirio ya gharama za ujenzi na vifaa zenye kukaribiana na uhalisia.Nataka nimjengee mapema iwezekavyo kuanzia sasa, tafadhali mchango wako wa mawazo unakaribishwa. Ahsanteni
[/SIZE]

farm-chicken-412.jpg

N.B. Samahani kwa usumbufu wowote utakao tokea ahsanteni[/QUOTE]
Mkuu kama alivyosema kituko hilo banda ni kubwa sana.Na gharama zake si haba nina uhakika hazitapungua Milioni 8 hivi...
Nilijenga km hilo (20 kwa 12) ngoja nipekue files nikuwekee mfano wa gharama nilizotumia..
Hili hapa chini
 
Attachments

  • IMG_20130916_122524.jpg
    IMG_20130916_122524.jpg
    324 KB · Views: 380
  • IMG_20130916_122515.jpg
    IMG_20130916_122515.jpg
    391.8 KB · Views: 352
Tatizo banda kama hilo uliweke kwenye maeneo ambayo hakuna vimbunga au upande miti mingi kulizunguka
 
Mkuu hiyo nyuma sio ndogo, ni kubwa sana, Kwa kukusaidia na makisio ya Kawaida tu ni Kama ifuatavyo:Hapa ni kwa mbao za treatedMbao za boma= 1080000/Mbao za kenchi 2x2 na 4x2=1584000Bati=1280000Floor (kokoto, mchanga, cement) =1300000Jumla ndogo= 5244000 ( bila kuweka gharama za wavu, mafundi, usafiri, misumari, ulinzi na gharama zingine zilizojificha) 1: Gharama inaweza kupungua kama ukinunua vitu reject pale Tazara- Buguruni, kuna kila kitu pale2:ukitumia mbao zisizokuwa treated unabidi upake dawa ya mchwa( dudu killer), na tatizo kubwa la hizo mbao huwa ni fupi, hivyo itakubidi ununue mbao mbili kwa kipande ambacho kingeweza kuzibwa na mbao moja ya treatedNimekosa muda, ningekuwekea na idadi ya material yanayotakiwa, lakini hilo banda sio chini ya 5.5 mil

Mkuu tafadhali nakuomba itafutie muda ningeitaji sana hiyo breakdown ya material, kuna mafundi bi mkubwa kawatafuta hivyo nikijua hii itanisaidia sana. Niokoe jahazi nisije nikapigwa mchanga wa macho.

Halafu kingine mkuu hizo mbao treated ni zile wanazopaka ile dawa nyeusi?
 
Tatizo banda kama hilo uliweke kwenye maeneo ambayo hakuna vimbunga au upande miti mingi kulizunguka

Hicho nilikifiria wakati naongea na bi mkubwa nikamwambia hicho kitu, sababu ukitazama hilo banda kwa pembeni wameweka nguzo za zege. Hapo kwenye kijishamba kangu ni tambarare hilo swala la upepo mzee lazima nikupe tano umeona mbali. MKuu lakini si ninaweza tumia yale mabomba ya chuma kwa pembeni badala ya hiyo zege?
 
Tupo wengi, hata mimi nina mpango wa 5x20m kwa ajili ya kuku na sample ndo hiyohiyo ila tu inabidi fundi atakwambia gharama. Mirunda au mbao treated zinalowekwa dawa zinakuwa kama kijani isiyokoza. Hiyo nyeusi ni za kawaida zinapakwa oily chafu. Sikushauri utumie zisizo na dawa kama nguzo. Nina kibanda kidogo nilitumia treated kama nguzo miaka 5 na bado ngumu. Ukiweza simamisha nguzo za zege kila pembe ingefaa sana. Vingine changanya na zako

Mama Joe kwanza nikushukuru, pia naomba nipate ushauri kutoka kwako. Hiki kibanda kwa sasa namjengea mama yangu sababu mimi sasa hivi sina mpango wa kufuga kutokana na shughuri zangu. Ila nataka nijenge kitu kizuri imara kitakachodumu hata miaka kumi ijayo sababu uwezi jua dunia hii ya leo ladba naweza kuanza kufuga mimi mwenye hapo baadae kama Mungu atatujalia uhai. Ikiwa kama nikijenga kitu imara kwa sasa nitasave hela kama hapo baadae nitaamuwa kufanya maamuzi ya ufugaji sababu nitakuwa sina tena gharama za ujenzi.

Swali sasa ni sawa kama nikitumia yale mabomba ya chuma kama nguzo badala ya zege? Kuna tofauti gani kwenye gharama hapo? Ushauri tafadhari
 
Ni kweli usemayo maana haya ya muda ndo tunatumia ila kama la kudumu huna mpango kulitoa baadae tumia aidha nguzo au chuma mimi nadhani fundi ndo atakueleza vizuri. Kwenye pembe nguzo ya zege inasaidia uimara toka kwenye msingi na linta, sasa sielewi chuma pekee itakuwaje. Chuma naona nzuri ktkt incase linakuwa pana sana yote fundi mzuri atakwambia iweje.
 
Mkuu MAKADIRIO YA GHARAMA Nilizotumia Katika Ujenzi wangu (20 kwa 12) zilikuwa;
1;UPAUAJI:
Bati(100) @ 12,000
Mbao 2*2 (80) @ 3,500
Mbao 4*2 (45) @7000
Miti Kurunge 9 @ 6000
Miti Mirunda 50@ 3000
Kofia+Misumari=100,000
TOTAL==2,099,000

2:MSINGI NA KUPANDISHA;
Tofali 800 @ 1000
Mchanga roli 6@ 90,000
Kokoto roli 1@ 160,000
Cement 50@ 13,000
TOTAL==2,150,000

3:MENGINEYO
Floor mchanga roli 6
Milango 2 @150,000
Chicken wire bunda 3@55,000
Ufundi (700,000)
TOTAL== 1,705,000

4;GHARAMA ZILIZOJIFICHA
Maji+usafiri n.k== 500,00

NB; Bati nilitumia used za pale Tazara.Pia kwenye kupaua nilitumia miti ile mirefu na mbao (kama wanavyopaua kwenye hoteli za makuti)....
Pia gharama za materials zinaweza zikawa juu huko bagamoyo kulinganisha na Dar.....
 
Back
Top Bottom