Waungwana kwa wale wenye uzoefu naomba muongozo tafadhali. Nataka kujenga banda kama hilo hapo chini lenye ukubwa wa (5X20). Nina kashamba kangu kapo Msata njia ya Bagamoyo nilitaka nimwekee mama yangu mradi aanze ufugaji wa bata mzinga. Hivyo nilitaka kujua makadirio ya gharama za ujenzi na vifaa zenye kukaribiana na uhalisia.Nataka nimjengee mapema iwezekavyo kuanzia sasa, tafadhali mchango wako wa mawazo unakaribishwa. Ahsanteni
N.B. Samahani kwa usumbufu wowote utakao tokea ahsanteni
Wanandugu naombeni mawazo yenu jamani,
Mkuu usiogope watakuja, bila shaka kiu yako ya hilo banda itaisha, vuta subira mamajoe Malila watakuja
Mkuu hiyo nyuma sio ndogo, ni kubwa sana, Kwa kukusaidia na makisio ya Kawaida tu ni Kama ifuatavyo:Hapa ni kwa mbao za treatedMbao za boma= 1080000/Mbao za kenchi 2x2 na 4x2=1584000Bati=1280000Floor (kokoto, mchanga, cement) =1300000Jumla ndogo= 5244000 ( bila kuweka gharama za wavu, mafundi, usafiri, misumari, ulinzi na gharama zingine zilizojificha) 1: Gharama inaweza kupungua kama ukinunua vitu reject pale Tazara- Buguruni, kuna kila kitu pale2:ukitumia mbao zisizokuwa treated unabidi upake dawa ya mchwa( dudu killer), na tatizo kubwa la hizo mbao huwa ni fupi, hivyo itakubidi ununue mbao mbili kwa kipande ambacho kingeweza kuzibwa na mbao moja ya treatedNimekosa muda, ningekuwekea na idadi ya material yanayotakiwa, lakini hilo banda sio chini ya 5.5 milWaungwana kwa wale wenye uzoefu naomba muongozo tafadhali. Nataka kujenga banda kama hilo hapo chini lenye ukubwa wa (5X20). Nina kashamba kangu kapo Msata njia ya Bagamoyo nilitaka nimwekee mama yangu mradi aanze ufugaji wa bata mzinga. Hivyo nilitaka kujua makadirio ya gharama za ujenzi na vifaa zenye kukaribiana na uhalisia.Nataka nimjengee mapema iwezekavyo kuanzia sasa, tafadhali mchango wako wa mawazo unakaribishwa. AhsanteniN.B. Samahani kwa usumbufu wowote utakao tokea ahsanteni
Mkuu hiyo nyuma sio ndogo, ni kubwa sana, Kwa kukusaidia na makisio ya Kawaida tu ni Kama ifuatavyo:Hapa ni kwa mbao za treatedMbao za boma= 1080000/Mbao za kenchi 2x2 na 4x2=1584000Bati=1280000Floor (kokoto, mchanga, cement) =1300000Jumla ndogo= 5244000 ( bila kuweka gharama za wavu, mafundi, usafiri, misumari, ulinzi na gharama zingine zilizojificha) 1: Gharama inaweza kupungua kama ukinunua vitu reject pale Tazara- Buguruni, kuna kila kitu pale2:ukitumia mbao zisizokuwa treated unabidi upake dawa ya mchwa( dudu killer), na tatizo kubwa la hizo mbao huwa ni fupi, hivyo itakubidi ununue mbao mbili kwa kipande ambacho kingeweza kuzibwa na mbao moja ya treatedNimekosa muda, ningekuwekea na idadi ya material yanayotakiwa, lakini hilo banda sio chini ya 5.5 mil
Tatizo banda kama hilo uliweke kwenye maeneo ambayo hakuna vimbunga au upande miti mingi kulizunguka
sema kiongozi St.Apolinary.
Nalog off
Hicho nilikifiria wakati naongea na bi mkubwa nikamwambia hicho kitu, sababu ukitazama hilo banda kwa pembeni wameweka nguzo za zege. Hapo kwenye kijishamba kangu ni tambarare hilo swala la upepo mzee lazima nikupe tano umeona mbali. MKuu lakini si ninaweza tumia yale mabomba ya chuma kwa pembeni badala ya hiyo zege?
Tupo wengi, hata mimi nina mpango wa 5x20m kwa ajili ya kuku na sample ndo hiyohiyo ila tu inabidi fundi atakwambia gharama. Mirunda au mbao treated zinalowekwa dawa zinakuwa kama kijani isiyokoza. Hiyo nyeusi ni za kawaida zinapakwa oily chafu. Sikushauri utumie zisizo na dawa kama nguzo. Nina kibanda kidogo nilitumia treated kama nguzo miaka 5 na bado ngumu. Ukiweza simamisha nguzo za zege kila pembe ingefaa sana. Vingine changanya na zako
Nimeiona kaka,udenda umenitoka kuiona hiyo mikuku natamani ingekuwa yangu,ni very useful post kwa kweli.Natumai umeona hii thread.