nikushukuru sana bwana Vicent, majibu ya maswali uliyouliza ni haya:-
1. Umri 57 yrs
2. Uzito 117 kgs
3. Urefu 1.97 M
4. Kazi ya ujenzi wa barabara- nafikiri ni mazoezi tosha.
5. Kuwaza kupo, hasa ukiwa mtu wa majukumu kifamilia.
6. Pombe, - Konyagi mix Cokacola,sio kulewa.
7. Kisukari - sina.
8. Macho - miwani ya kusomea.
9. VIPIMO nilipima kwenye hospital ya wachina (TIENS) na kipimo cha ki-umeme kwenye kiganja wakaona matatizo :-
a. Uti wa mgongo.
b. Allergy ya ngozi.
c. BP.
d. Figo.
e. Artteries.
f. Macho.
g. Nk.
nimekuelewa, hivyo vipimo vya kichina sivielewi, ila uzito wako ni mkubwa una BMI ya 30.15
kg/m[SUP]2 .
[/SUP]kawaida inatakiwa kuwa 1
8.5 to 24.9kg/m[SUP]2 .
[/SUP]Kazi yako si mazoezi tosha, usifikilie hivyo, yengekuwa mazoezi tosha basi uzito ungelipungua. konyagi na cocacola ni vinaongeza sukari mwilini, hasa cocacola na hivyo vinaweza sababisha pressure (hasa pombe ni njia moja wapo ya kusababisha pressure, kwani hufanya mishipa ya damu kusinyaa na kuongeza msuko wa damu katika mishipa na hata taratibu huharibu moyo, na baadae kupatwa na magonjwa ya moyo.
ningekushauri upime vipimo hivi, halafu unitumie ili niweze kukupatia ushauri zaidi. s-creatinin,cholesterol, s-LDL, S-HDL, ALAT, ASAT, S-GT,S-GLUCOSE, URIC ACID, Albumin, ECG, URINALYSIS, TSH, T4,
Na kama unavuta acha. baada ya vipimo hivyo twaweza ongea vizuri. pressure husababisha magonjwa ya moyo. figo kutofanya kazi vizuri na hata kupata kiharusi kama hutibiwi. kwa ushauri wangu kuwa mwangalifu. zingatia niliyo kuwaambia. kwa majibu yako hapo juu naona wew huijui hatari ya pressure. ukisikia watu wanaangunga ghafla na kuparalyse au kufa jua wengi chanzo ni pressure. chunga afya yako. lala mapema , baada ya kzi pumzika na fanya mazoezisi ya nguvu sana,