Sijaelewa uhusiano wa kutolala na 'ugonjwa' unaoufikiria unao, Rheumatism! Labda ni kwa sababu mtu fulani katika familia/ukoo anao na wakati anao alikuwa na shida ya usingizi.
Kwa maelezo yako inawezekana hali yako ni kutokana na mfumo wa maisha(Mwanafunzi), na hivyo kuwa na ratiba fulani ya kusoma ambayo mwisho wa siku mwili wako huzoea na kuwa unakosa usingizi huo..pili mwili hufanya njia ya adjustment/regulation wakati wa Stress/Msongo na hii oia huweza kusababisha kutopata usingizi vyema, na kutofanya kazi vizuri siku inayofuata.
Lakini kwa hali hii, Sijaona dalili ya kusema unashida ya Rheumatism...Wakati fulani kukosa usingizi ni tatizo kiafya, yaani INSOMNIA, na hii pia inaweza kuwa Early Insomnia, Late Insomnia n.k Nikimaanisha wapo watu ambao wana maisha ya kawaida ambayo hayawahitaji kuwaamsha kwa ulazima wakati wa usiku na usingizi kupotea, lakini ifikapo muda wa alfajiri(hasa saa kumi) hukosa usingizi "usingizi kupaa" kabisa na kufanya wakae macho.
Hata hivyo, sidhani kama hili ni tatizo hapa kwa sababu ya mtindo/mfumo wa maisha unaokulazimu wakati fulani kuamka muda huo.
Adjustment ya ratiba yako, ni muhimu katika shida uliyoisema, na endapo hali itazidi nakushauri ufike hospitali.