Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..!

Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..!

Penzi halina uhusiano wowote ule na Pesa.

Jamaa hajampenda huyo mdada.

Mdada achape lapa, atapata anayempenda.:smash:
 
Tena hawachelewi kukwambia eti 'wewe ni mwanaume suruali tu'. nani anataka huo ujinga, akhaaaaaaaaaaa! Mwishowe unakuja kutumwa kwenda sokoni kununua viungo vya pilau. Acha kabisa hawa mademu wa kibongo wenye nazo, utazodolewa mwanaume mpaka utamani ardhi ipasuke.

Tunawafahamu hao wanao pinga hapo juu hawajakutana nayo haya.
Mwanamke wa kibongo akipata ****** yanalia mbata heshima kwa mmewe inashuka kabisa.
 
Huyo wa zamani kweli,...
zamani ulikua unao kwa pale unapokua fiti kwa kipato kama mwanaume,...
siku hizi unaangalia mwanamke alotimia mfukoni,....

Kapoteza bahati,but amani ya moyo ndio dereva mwema.Hongera zake.
 
huyo binti alimdanganya mwenzie. dada zetu jaribuni kuwa wakweli.hadi amuulize anaishi na nani ujue kaona suruali humo ndani. tuseme alikua hajamwambia mda wote kwamba anaishi peke yake? hayo ya kusema amekimbia sababu ya kipato cha mwanamke siyo kweli. hayo ya kipato ni maneno ya mwanamke ili kupoteza maana na kujiondoa katika lawama. madada kuweni waminifu. over
 
Kweli ubinadamu ni kazi, ukiwanazo wanakukimbia usipokuwa nazo wanakupa majina kibao, sasa sijui tufanyaje
Habari zenu wapendwa,
Kuna mkaka ni mkazi wa dar ila anafanya kazi mgodini huko mwanza huku anakuja kila baada ya miezi miwili,Alikutana na mdada huko mwanza Mdada anafanya kazi huku dar kule alienda kikazi,wakapeana kontakt, na mawasiliano yakaendelea na wakawa wapenzi.

Kwa kipindi cha miezi minne ya mahusiano yao hakuna aliyekua anajua kwa mwenzie,basi wakapanga jamaa atakapokuja dar wakaoneshane makwao,basi jamaa akarudi dar ijumaa iliyopita km kawa wakakutana na jmosi jamaa kampeleka mdada kwake tabata wakashinda huko wakapika na kupakua.

Jpili mdada naye akampeleka jamaa kwake maeneo ya Sinza hapo ndio balaa lilipoanzia kwan muda wote wakiwa pale yule mkaka alikuwa hana raha mwenzie akamuliza kulikon mbona ulikuja vizuri,yy akamuuliza pale anaishi na nani akamwambia mbona nilishakwambia naishi peke yangu.

Akamwomba amwonyeshe slip yake ya mshahara mdada akapigwa butwaa ila akamwonyesha kumbe kaharibu jamaa kanyanyuka na kuondoka akiwa amekasirika mdada hakumwelewa akambembeleza bila mafanikio,usiku wake jamaa akamtumia bint msg kuwa hamtaki tena,kwa sababu anahisi huyo mdada atamtawala maishani kwa vile kwanza ana kipato kikubwa,na ameshajijenga sana kimaisha,hivyo ni rahisi yeye kutokuwa na sauti ndani ya nyumba,au huyo dada anaweza kumwaga wakati wowote na kutoka na wenye uwezo km yy.

Mpaka ninavyoandika huu uzi jamaa hapokei simu na jana kaondoka kurudi mwanza,dada watu kachanganyikia alishampenda jamaa kupita kiasi hata hajui cha kufanya!

Asa mi nauliza hivi nyie wanaume hivi binti kuwa na kipato kikubwa kuliko mwanaume ni kweli ni tatizo kwenye mahusiano?
Na dada afanyaje ili jamaa aelewe na waendelee?
 
Kweli Mzazi, asilimia kubwa ndo hivyo, unajua haya mambo bado yanenda na mfumo uliopo ndo maana hata hapa ukiuliza mabinti wenyewe hua wanasema wanapenda kuolewa na Mtu alie mzidi umri, na sababu wanasema mwanaume ndo kichwa cha Familia sasa wewe na laki tatu zako unaleta dagaa wakati mama anapitia super market kila siku?

Kuwa kichwa maana yake ni kufanya maamuzi yote kwa kujiamini,hata kama huna kazi na mkeo analipwa mil 20 kwa mwezi,sasa naendelea kumkubali babu Aspirin na uzi wake!Hebu kausome!
 
Malezi ya mfumo dume yana nguvu sana, ogopa sana mwanaume aliyelelewa na kuaminishwa kwamba ni mwanaume pekee mwenye mamlaka ya kumiliki mali achilia mbali elimu............................ Ndyoko ni mfano mzuri sana wa jambo hili................LOL
 
Do u belive mfumo dume exist,or is an excuse kwa wanawake wasiojiamini?
 
Penzi halina uhusiano wowote ule na Pesa.

Jamaa hajampenda huyo mdada.

Mdada achape lapa, atapata anayempenda.:smash:
Kwanza shikamoo babu,
Yani inawezekana kbs,kipatp tu akimbie?
Asante babu kwa ushauri.
 
Malezi ya mfumo dume yana nguvu sana, ogopa sana mwanaume aliyelelewa na kuaminishwa kwamba ni mwanaume pekee mwenye mamlaka ya kumiliki mali achilia mbali elimu............................ Ndyoko ni mfano mzuri sana wa jambo hili................LOL
Unacho ongea ni kweli kabisa, Bora kasepa kuliko kukosa Amani ya moyo,
Maana ndo alivyo lelewa hivyo ndo maana simshangai jamaa
 
Tunawafahamu hao wanao pinga hapo juu hawajakutana nayo haya.
Mwanamke wa kibongo akipata ****** yanalia mbata heshima kwa mmewe inashuka kabisa.
Khaaaa,makubwa!
Kwa hiyo hata ww ikitokea mkeo akapandishwa cheo na maalawansi yakaongezeka na kupita kiapto chako utamwacha?
 
Mopuuzi kweli huyo, ana mawzo ya mwaka arobaini na mbili.....sidhani kama ana akili timamu kweli, ngoja nitafute tusi zuri maana mijtu ya nmana hii ndio inayoendeleza mfumo dume halafu haikawii kulalamika. Pumbafu kabisa
 
Huyo wa zamani kweli,...
zamani ulikua unao kwa pale unapokua fiti kwa kipato kama mwanaume,...
siku hizi unaangalia mwanamke alotimia mfukoni,....

Kapoteza bahati,but amani ya moyo ndio dereva mwema.Hongera zake.
Hata mie naona huyu wa zamani badala afurahie watasaidiana kimaisha yy anakimbia!
Asante mkuu kwa maoni.
 
huyo binti alimdanganya mwenzie. dada zetu jaribuni kuwa wakweli.hadi amuulize anaishi na nani ujue kaona suruali humo ndani. tuseme alikua hajamwambia mda wote kwamba anaishi peke yake? hayo ya kusema amekimbia sababu ya kipato cha mwanamke siyo kweli. hayo ya kipato ni maneno ya mwanamke ili kupoteza maana na kujiondoa katika lawama. madada kuweni waminifu. over
Wala hakuona suruali,ishu ni kwamba baada ya kuona thaman za mle ndani hakuweza kuamin gafla kuwa ni uwezo wa yule binti,
Ndio maana akataka kuthibitisha kwa kuomba slip ya mshahara ili kulinganisha na vitu anavyona mle ndani,
Na alipopata uhakika ndio akaona binti kamuacha mbali na kuamua kukimbia!
 
Kweli ubinadamu ni kazi, ukiwanazo wanakukimbia usipokuwa nazo wanakupa majina kibao, sasa sijui tufanyaje
Mwenangu hawa viumbe sijui wanataka nn? mbona hawana jema jamani?
 
Back
Top Bottom