Msaada tafadhali: Kisaikolojia nahisi mimi kumtongoza mwanamke ni kama najishusha, na najidhalilisha.

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Sijui hii hali kama kuna wengine Ishawahi wakuta, Umri wangu Niko kwenye late 20's miaka ya nyuma nilikua tongoza tongoza, aisee lakini sasa sijui nimekuaje, kama mwaka uliopita nimetongoza mdada mmoja tu, the whole year.

Mimi sio domo zege, sina stress kubwa/msongo wa mawazo, sina aibu ya kuongea na mwanamke, ila nikiona mwanamke ninaemtaka, nkifikiria kwenda kumtongoza, akilini huwa naona kama ntampa kichwa, yani naona kumtongoza ni kwenda kujichoresha, Na kujishusha thamani, na kujivua nguo mbele ya binadamu mwenzangu tena hadharani..nawaza kama kutongoza sio kujidhalilisha, mbona wanawake hawatufati kututongoza sisi wanaume, that means wanawake wanajua kutongoza ni kujishusha, ivo nakausha..

kuna mtu mwingine ashawahi experience hii, maana logically naona kwangu hii ni shida aisee..najiona kama naenda against nature

NB: Mashine inafanya kazi vizuri, mm ni mwanaume straight, maana baadhi watu humu hawakawii kuniita upinde..
 
Kwani bado kuna kutongozana sasa hivi?
 
Una nyota ya utajiri Endelea kupambana. K haijawahi kumwacha mtu salama
 
Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
 
Kama unahisi unajishusha si utongozwe wewe tu? Unasubiri nini kutongozwa?
Hapo kwenye N.B ndiyo umekaribisha mashaka zaidi. Wanaume huwa hawajitetei hivyo. Either wewe ni KE au kweli una hilo tatizo
 
Tongoza Mwanamke mwenye vitu vya ku-offer kwako na sio Ngono tu, sex is overrated only u need is to live ur life simply
 
Uoga wako ndiyo umasikini wako
 

Ungeanza na utangulizi na maana ya neno "kutongoza"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…