Habari wakuu,
Ninaomba kupewa muongozo au msaada kua kati ya kozi hizo tatu za kilimo ipi ina tija na ni nzuri haina usumbufu mwingi mbeleni kwa pale SUA.
Pia, soko lake zuri iwe kwenye kujiajiri au kuajiriwa
Nahitaji kuchukua moja wapo hapo nikipewa faida na hasara itanisaidia kutambua wapi nikae.
Habari yako mkuu, nitachangia Kwa uelewa wangu juu ya swali lako, Kwanza kabisa ulitakiwa useme Agricultural General, Animal science labda na Horticulture ila sio crop science
Haya Turudi kwenye mada, Kwanza kabisa kaa ujue kuwa hivi sasa kuna uhaba mkubwa wa ajira Nchini kwahiyo toa dhana ya kusoma ili uajiriwe, at least unatakiwa uchague course ambayo ata ukimaliza unaweza kujiendeleza kiuchumi wewe mwenyewe na shughuri zinazohusu fani yako
Ya Kwanza me ningekushauri uchague General Agriculture, maana ina uwanda mpana sana kuhusu kilimo cha Aina zote za mazao lakini pia ni rahisi kujiajiri ata kama utakosa Ajira ya permanent, kwakuwa utakuwa na elimu hivo utaweza kutumia mtaji mdgo/kipato kidogo kwenye implementation yako kwakuwa unajua ufanye nini katika Ardhi ndogo Kwa mtaji mdgo ila upate mavuno yenye Tija, lakini pia unaweza kutumia elimu yako kwenye kuelimisha jamii ya wakulima Kwa kuandaa seminar elekezi na kupitia huko kuna baadhi ya watu wanaweza kuwekeza pesa zao kwenye elimu yako then wao wakasubiri matokeo
Ya pili ningekushauri ukasome Horticulture, hii course tunaweza kuiita ni course mtoto wa General Agriculture, maana hii ina deal na uzalishaji wa mboga mboga, Matunda, Gardens, Kwa dunia ya Leo watu wamejua umuhimu wa kula mboga za majani na Matunda kwahiyo kupitia elimu yako utaweza kuona fursa na kuifanya Kwa usahihi zaidi na ili kuongeza thamani ya bidhaa zako, utakuwa tofauti na ambao wanalima Tu Kwa mazoea, hii biashara ni sawa na biashara ya chakula haiwezi kukosa soko daima
Na mwisho kabisa nisingekushauri kusoma Animal science, maana haina wigo mpana kwenye kujiajiri maana usipoajiriwa serikalini basi yakupaswa uajiriwe katika makampuni ya kutengeneza vyakula vya mifugo na kumbuka mtaani wapo wengi Tu ambao hawajapata mashavu na wanashindwa kujiajiri kwakuwa kufanya Mambo Yao Kwa tija kunahitaji pesa nyingi kidogo tofauti na mtu wa General Agriculture na Horticulture,tofauti na hapo basi yakupasa kusoma na ukiwa na plan ya kuja kuanzisha kampuni ya chakula ata wa kuku wa kienyeji maana wa kisasa teyari kuna kampuni kubwa nyingi ambazo kushindana nazo ni ngumu
Mwisho kabisa kitu cha msingi ni kuangalia wewe unapenda kusoma nini Kati ya hizo course, kuna tofauti kubwa sana Kati ya mtu ambae anasoma kitu anachokipenda na Yule ambae anakisoma Kwa lengo la kuangalia opportunity, kama utakuwa na marks nzuri basi sio vibaya ukaiweka na BVM ukajaribu bahati yako, uzuri wake ni kwamba loan ni 100% na kozi ya miaka mingi kwahiyo kama utatumia vizuri bumu lako basi unamaliza ukiwa na elimu lakini pia ukiwa na pesa ya kuweza kuja kufanya Jambo uraiani, lakini pia ndio course pekee ambayo ni ngumu kukuta mtu analia lia na Ajira