Tafadhali wapendwa, tarehe 22 Septemba niliona tangazo la ajira ya Field Officer katika NGO ya AIDS Care Foundation. Baadaye nilitumiwa barua pepe kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa ajira.
Hata hivyo, katika hatua hiyo nimeelekezwa kufanya assessment kupitia kampuni nyingine, na cha kushangaza zaidi nimeambiwa ili nifanyiwe assessment hiyo natakiwa kulipa kupitia USSD Sh 60,000, Sh 70,000 au Sh 80,000.
Naomba msaada kutoka kwa mtu yeyote anayefahamu kuhusu mchakato huu au aliyewahi kupitia hatua kama hii. Je, hii ni sehemu halali ya mchakato wa ajira au kuna uwezekano wa kuwa ni utapeli?
Mwenye taarifa au uzoefu kuhusu suala hili, tafadhali atupe mwanga.