Msaada Tafadhali: kwa yeyote anayeweza kunisaida kwa hili

Slow learner

Member
Joined
Jul 6, 2019
Posts
18
Reaction score
8
Habari zenu wakuu.

Nimezingatia kauli ya wahenga isemayo "mficha maradhi mauti umuumbua", binafsi nahitaji msaada wa kimawazo kutoka kwenu wataalamu.

Umri wangu ni mdogo tu,lakini nimekuwa nikifanya shughuli mbalimbali za utafutaji,nimekuwa nikijiwekea malengo fulani kutokana na shughuli ninazo zifanya.

Tatizo ni kuwa ikitokea nimeacha shughuli hiyo lazima na malengo yabadilike(lazima nibadilishe malengo yangu).mfano nikiwa dereva wa magari najiwekea malengo kuwa siku moja nije kumiliki kampuni ya usafirishaji wa mizigo,au nikiwa mwalimu natamani siku moja nifungue shule yangu binafsi.

Kwa ufupi ni kwamba;sina lengo kuu la maisha.

NB:-Nimekuwa si mvumilivu katika kuyasubiri mafanikio
- Nimekuwa mwepesi wa kufanya maamuzi ya moyoni na mdomoni but si kwa vitendo
- Nimekuwa si mtumiaji mzuri wa pesa(flow management)
- Nimekuwa nafanya maamuzi kwa haraka sana na baadae nayajutia
- Nimekuwa nikiwashauri watu wengi kuhusu matumizi ya pesa na mbinu za utafutaji na wanafanikiwa but nikifanya mimi naangukia pua
-Binafsi ni mwoga wa kufanya maamuzi yanayoonekana kwa watu
-Yote kwa yote ninaogopa sana kukosea

Nina wafuatilia public motivators wengi tu,na ninaiambia nafsi yangu it's to change lakini nikikaa masaa mawili au matatu nasahau kila kitu na mawazo yanahamia upande mwingine.
Msaada wenu please! 🙏🙏🙏
Njia yoyote unayohisi itanisaidia niambie tafadhali,japo naijihisi mimi ni "MPUUZI"😎😎
 
Nani akiyesema inabidi uwe na Lengo moja kwamba kumiliki Shule basi hilohilo, kampuni ya usafi basi hilohilo...kwani hupendi vyanzo vingi vya mapato.

Malengo hata ukiwa nayo 8 hakuna tatizo chamsingi uandike malengo yako na ujue unaanza na lipi.
 
Jambo la kwanza badili jina lako na usijiite slow learner maana majina yanaumba na yanakutengenezea mtazamo wa wewe kuwa hivyo kwakuwa tayari kwenye ubongo wako unaamini you're a slow learner.

Kuna kusudi kuu la maisha ambalo kila mmoja analo. Hakuna ambaye yupo duniani kuishi na kupita tuu, kuna kitu ambacho wewe ulipaswa kukamilisha kabla ya kuondoka kwako hapa duniani.

Jambo hilo linatofautiana kwa kila mmoja na wapo ambao tayari wanajua nini walizawa kufanya katika maisha kabla ya kuondoka duniani.

Sasa ili kufikia malengo hayo zipo njia mbalimbali za kukufikisha katika lengo kuu. Njia hizo ndo hayo malengo madogomadogo, malengo ya muda mfupi ambayo unakuwa nayo kwa lengo la kufikia hatua fulani ili kukuwezesha kufikia lile lengo kuu ulilonalo katika maisha kiujumla.

Tatizo lako ni moja tu, bado hujajua kusudi au lengo kuu la maisha yako ndiyo maana unahamahama, yaani kila kazi unayopata unahisi ndiyo litakuwa kusudi kuu katika maisha yako na unajiwekea malengo ya muda mrefu kwa kazi ya muda mfupi.

Nikupe huu mfano, mimi mwenyewe binafsi nina malengo ya kuwa na kampuni ya utoaji ushauri katika maisha, biashara na Teknolojia na hata katika nyanja mbalimbali. Ila lengo kuu ni kuwa mtoa ushauri kiujumla. Naomba unielewe vizuri, lengo kuu ni kuwa "mshauri" ila ni katika hizo aspects hapo juu.

Nina malengo madogomadogo yakayonifanya kufikia lengo hilo kuu, nauza vitabu vya shule na nakala mbalimbali za wanafunzi zote online (softcopy documents), nafundisha wanafunzi masomo ya Physics Chemistry na Mathematics, nafanya digital marketing hasa upande wa social media marketing, nafanya biashara ya Mchele (delivery ni bure kabisa) na shughuli zingine, ILA!! Utofauti wangu katika kuyafanya hayo yote ni "sababu" za mimi kufanya hizo shughuli zote na mengine ambayo sijayataja hap.

Target yangu katika kazi zote hizo ni moja tu, natafuta uzoefu katika maeneo ambayo ndiyo kusudi langu kuu, (kuwa mshauri) .

Naelewa siwezi mshauri mtu kuhusu biashara wakati sijawahi fanya biashara, siwezi mshauri mtu kuhusu mahusiano wakati sina familia, siwezi mshauri mtu kuhusu masuala ya Tehama wakati hakuna faida niliyowahi kuipata au hata kazi niliyowahi kufanya kupitia Teknolojia kiujumla.

Yote katika yote shughuli hizo zote ni kama malengo ya muda mfupi ili kufikia kusudi kuu la kuwa mshauri mwenye uzoefu katika maeneo anayoshauri. Hivyo nafanya nikitambua KWANINI nafanya.

Narudi kwako, ukitambua kusudi lako halisi itakuwa rahisi sana kutambua KWANINI unahama kazi fulani, ili kutokuweka mategemeo Makubwa katika kazi hiyo unayoifanya kwasasa kwakuwa unaelewa siyo kusudi lako bali ni njia kufikia lengo kuu.

Kaa chini JIULIZE nini kusudi lako katika maisha yako, nini lengo lako kuu katika maisha yako kiujumla, unataka ufanye nini katika maisha ndipo utoweke duniani. Ukipata majibu basi itakuwa rahisi sana kujua sababu za wewe kufanya kazi fulani hivyo kuepusha kujiwekea malengo makubwa eneo ambalo siyo sahihi katika maisha yako.

Ukijua lengo lako kuu ambalo upo tayari kuwekeza muda na nguvu ili kulifikia itakuwa ni rahisi sana kutambua kwann unafanya hicho unachokifanya.

Kipo kitabu ambacho nakiandaa (ISHARA 102, WEWE NI WA TOFAUTI)
Kama utahitaji kufuatilia zaidi na kujifunza,kwasasa natoa hiyo hiyo series ya hizo ishara zote 102 kupitia account page yangu ya facebook ,inayojulikana kama
"musabskilld consultants" utapata muendelezo mzima.

Kama upo instagram tupo pia kama @musabskilldconsultants
 
Mkuu hayo uluondika hapo kuuza mchele, kuuza notes nk Sio malengo au malengo madogo bali Mikakati ya kuelekeza lengo.

Malengo uliyotaja ni hilo la Ushauri tu na hiyo ndio Mikakati ya kuiendea lengo.
 
Asante kwa ushauri mkuu,nitajitahidi kuufanyia kazi
 
Mkuu,mara nyingi niapanga kufanya mambo mengi lakini namna ya kuyatekeleza ndo mtihani,najishangaa kwani nimewahi kumpa mtu wazo la biashara na namna ya kulitekeleza aka win,but nilipo jaribu mimi ilikuwa ni balaa,na kama nilivyo eleza mwanzo"Mimi si mvumilivu katika kusubiri mafanikio"
 
Back
Top Bottom