Po
Habari ndugu zangu!
Gari aina ya Noah Townace, Old model (Automatic)... Speedometer yake haisomi kabisa, na imeecha ghafla! JE, NICHEKI NINI HASA? (Ninayo Idea ya umeme wa magari ila sijawahi kujua operation ya speedometer)
Nawasilisha
Pole sana mkuu..kama una idea ya umeme wa magari umeshindwaje kujua operation yake??.
Hapo kuna aina mbili au mambo mawili au matatu..
Kuna aina 3 za speed meter.
1:speed meter ya cable?? Hii husomwa au someshwa na cable
2:ya umeme na maanisha kwenhe gearbox yako nyuma kabisa mwishoni karibia na linapo funga properal kuna kuwa na sensor ya waya 3..
Kama itakuwa inatumia hii nenda moja kwa moja angalia hiyo sensor chomoa boya/connector yake ukiwa umelishika linakutazama ww kuanzia upande wako wa kushoto pini ya kwanza ni 12V+ pin ya pili ni 12V- ya mwisho ni signal ya kwenda kupandisha speed meter.hivyo pima kama hivyo viwili namba 1 na 2 vipo kama vipo weka tester yako kwenye ground then gusisha gusisha kwenye pin #3 unagusisha na kuachia kwa haraka na mara nyingi speed meter lazima inyanyuke kama isipo nyanyuka kagua fuse zote na pima continuty ya waya pin#3 kutoka kwenye connector ya sensor mpaka kwenye dash board..kama vyote viko powa change dash board/clustet.
3.speed meter inayoendeshwa na ABS hapo kama ukiangalia kwenye gearbox hakuna sensor wala cable basi inatumia au speed meter inaendeshwa na mfumo wa ABS.
Angalia taa ya ABS inawaka?? Kama ndio basi shughulikia mfumo wa abs mambo yatakuwa byee.inshort hapo pima fault code manually ukipata fault kagua kweli kama imekusomea sensor ni nzima au laa??.i flush the pima fault ikiondoka test gari uone speed meter inapanda au laa..
Aina hii huwa inakuwa pasua kidogo kwa mafundi wengi lkn hapa ndio mahali pake mpaka diagram ya ECU ABS na fault code zote utapewa ukihitaji .kwa kuwa umesema unauelewa na ufundi wa umeme wa magari..naamini itakubali. Au ukitaka utanicheki #0627136700